Pata taarifa kuu
HAITI-SIASA

Haiti: Moja wa wahusika wakuu wa mauaji ya rais Jovenel Moïse akamatwa

Polisi ya Haiti imetangaza kwamba imemkamata mmoja wa wahusika wakuu wa mauaji ya Rais Jovenel Moïse, raia wa Haiti ambaye mamlaka inamshutumu kwa kuajiri mamluki ili kumwondoa Moïse mamlakani na kuchukua nafasi yake.

Mkurugenzi Mkuu wa Polisi Haiti Leon Charles akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Port-au Prince, Julai 11, 2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Polisi Haiti Leon Charles akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Port-au Prince, Julai 11, 2021. Valerie Baeriswyl AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa polisi amesema mtuhumiwa, Christian Emmanuel Sanon, 63, aliwasili Haiti mapema mwezi Juni akiwa ndani ya ndege ya kibinafsi, akiambatana na mmoja wa maafisa wa usalama, kwa lengo la kuckuwa madaraka.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, amesema kuwa sababu za Christian Emmanuel Sanon zilikuwa za kisiasa na kwamba mtu huyo alikuwa akiwasiliana na "wahusika wengine" wa mauaji hayo.

"Kazi ya washambuliaji hawa hapo awali ilikuwa kuhakikisha usalama wa Emmanuel Sanon, lakini baadaye ilibadilika," amesema Leon Charles.

Tangu kuuawa kwa rais wa Haiti, hali ambayo imeongeza mgogoro nchini humo, polisi wa Haiti wamewakamata raia 18 wa Colombia na watatu wa Marekani wenye asili ya Haiti, amesema mkuu wa polisi. Raia wengine watano wa Colombia wako mafichoni, akmeongeza, na wengine watatu wameuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.