Pata taarifa kuu
HAITI-HAKI

Waziri Mkuu wa Haiti aonya wale wanaotaka kupotosha kesi ya mauaji ya Jovenel Moise

Waziri Mkuu wa Haiti anashutumu "mbinu zinazofanywa" katika uchunguzi wa mauaji ya rais Jovenel Moïse ili kupotosha kesi hiyo, baada ya kualikwa kufika mahakamni. Amesema alizungumza kwa simu na mmoja wa watu waliotafutwa saa chache baada ya mauaji.

Waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry.
Waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry. Valerie Baeriswyl AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Ujanja wa kujibadilisha kesi hii ili kuzua mkanganyiko na kuzuia haki kufanya kazi yake kwa utulivu haitapita," amesema Ariel Henry.

"Wahusika halisi, walitekeleza na wadhamini wa mauaji hayo ya kikatili ya Rais Jovenel Moïse watapatikana, watafikishwa mahakamani na kuadhibiwa kwa uhalifu wao," ameongeza.

Ijumaa jioni, Wakili Bed-Ford Claude, kamishna wa serikali ya Port-au-Prince (sawa na mwendesha mashtaka) alimwalika Bwana Henry kufika ofisi ya  mashtaka Jumanne, akisema alizungumza kwa saa chache baadaye mauaji ya Jovenel Moïse, na mmoja wa watu wanaotafutwa katika uchunguzi unaoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.