Pata taarifa kuu
HAITI

Haiti: Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi yaongezeka hadi 2,189

Haiti inakadiria mamia ya maelfu ya watu ambao wanahitaji msaada wa kibinadamu. Lakini ni vigumu kufika katika baadhi ya maeneo.

Maafisa wa uokoaji wanajaribu kupata kutafuta watu waliofunikwa vifusi vya nyumba zilizoporomoka kufuatia tetemeko la ardhi huko Les Cayes, Agosti 17, 2021.
Maafisa wa uokoaji wanajaribu kupata kutafuta watu waliofunikwa vifusi vya nyumba zilizoporomoka kufuatia tetemeko la ardhi huko Les Cayes, Agosti 17, 2021. AP - Fernando Llano
Matangazo ya kibiashara

Makundi yenye silaha yaliyokuwa yakiendesha ukatili wao nchini Haiti yamsitisha uhalifu huo kwa mauda kutokana na tetemeko la ardhi, lakini hii hairuhusu mashirika ya kibinadamu kutoa misaada muhimu kwa walengwa.

Mvutano ni mkubwa na baadhi ya Wahaiti waliokumbwa na tetemeko la ardhi wanaishi katika maeneo ambapo ni vigummu kufika. "Tuna watu wapatao 600,000 walioathirika moja kwa moja na wanaohitaji msaada wa haraka wa kibinadamu," amesema Jerry Chandler, mkurugenzi wa kikosi cha Ulinzi na Usalama wa Raia wa Haiti, kutoka kituo cha kitaifa cha operesheni za dharura huko Port-au-Prince.

“Tumelazimika kutafuta njia za kuhakikisha usalama, hali ambayo bado ni changamoto kubwa. Tunajua kwamba kulikuwa na tatizo katika kuondoka kusini mwa Port-au-Prince, huko Martissant lakini tatizo hili linaonekana kuwa limetatuliwa, kwani tumeweza kuzuru eneo hilo siku mbili zilizopita, "amesema.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Juni, hakukukuwa na usalama wa barabarani,  kulikuwa kukitokea mashambulizi au kusikika milio ya risasi baada ya kilomita mbili huko Martissant, eneo masikini la mji mkuu wa Haiti, lililoathiriwa na mapigano kati ya magenge ya dawa za kulevya. Kufuatia tetemeko la ardhi ambalo liliathiri nchi hiyo, risasi za mara kwa mara na mashambulio dhidi ya magari vimekoma, mamlaka zinasema, bila operesheni ya polisi kufanyika ili kudhibiti tena eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.