Pata taarifa kuu
HAITI-SIASA

Haiti: Uchaguzi waahirishwa hadi Novemba 7

Uchaguzi nchini Haiti umeahirishwa hadi Novemba 7, kulingana na vyombo vya habari nchini humo. Hatua hiyo inakuja baada ya mauaji ya rais Jovenel Moïse mwezi uliopita.

Hivi karibuni Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Ariel Henry aliahidi kufanyika uchaguzi wa haraka wa taifa hilo.
Hivi karibuni Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Ariel Henry aliahidi kufanyika uchaguzi wa haraka wa taifa hilo. REUTERS - RICARDO ARDUENGO
Matangazo ya kibiashara

Nyaraka ambazo zinaonekana kutolewa na serikali, zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii Jumatano, zinaeleza kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais na wa wabunge, na pia kura ya maoni ya kikatiba, ambayo hapo awali ilipangwa kufanyika Septemba 26.

Kulingana na shirika la habari la REUTERS ni vigumu kuthibitisha ukweli wa hati hizo. Baraza la uchaguzi Haiti halikuweza kuzungumza chochote kuhusiana na habari au nyaraka hizo.

Hivi karibuni Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Ariel Henry aliahidi kufanyika uchaguzi wa haraka wa taifa hilo.

Henry alisema mpango wa serikali yake ni kufanikisha uchaguzi huru, wa kuaminika, wenye uwazi ambao utawashirikisha wapiga kura wengi huku akisisitiza hitaji la usalama nchini humo.

Takribani watu 28 wametiwa mbaroni kutokana na tuhumza na mauwaji ya Jovenel Moïse, wakiwomo wanajeshi 18 wa zamani wa Colombia, pamoja na afisa wa ngazi ya juu wa polisi ambae alikuwa akiongoza timu ya usalama wa rais Moise. Lakini bado serikali inaendelea kuwasa watuhumiwa wengine akiwemo, kiongozi wa waasi wa zamani, seneta wa zamani wa Haiti pamoja na jaji wa Mahakama Kuu wa Haiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.