Pata taarifa kuu
HAITI-HAKI

Jaji anayechunguza mauaji ya Jovenel Moïse aachia ngazi

Haiti inaendelea katika sintofahamu na mvutano zaidi ya mwezi mmoja baada ya watu wenye silaha kuvamia makaazi ya rais Jovenel Moïse na kumuua. Ucunguzi kuhusu mauaji hayo bado ni tatizo na kwa kutoa mwanga juu ya shambulio hili si kazi rahisi: jaji aliyeteuliwa kuongoza uchunguzi wa mauaji hayo, amesema hataendelea na kesi hiyo.

Mtu huyu akiangalia picha ya rais wa Haiti hayati Jovenel Moise wakati wa mazishi yake huko Cap-Haitien, Julai 23, 2021
Mtu huyu akiangalia picha ya rais wa Haiti hayati Jovenel Moise wakati wa mazishi yake huko Cap-Haitien, Julai 23, 2021 REUTERS - RICARDO ARDUENGO
Matangazo ya kibiashara

Siku nne baada ya kuteuliwa, jaji Mathieu Chanlatte ameiarifu rasmi mahakama ya Port-au-Prince mara ya kwanza kwamba hataendelea na kesi hiyo kwa "sababu za kibinafsi".

Uamuzi huu wa haraka umewashangaza wengi, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa Chama cha Mahakimu nchini Haiti, Jaji Jean Wilner Morin.

"Nilikuwa nimesema kuwa haitakuwa rahisi kwa jaji Chanlatte kuongoza kesi hii wakati tunajua kuwa bado ana gari moja inayojulikana na wakaazi wa mji huu wakiwemo wahalifu na kwamba hana maafisa wa kumlindia usalama. Kwa hivyo ni ngumu sana kwa jaji huyo kuendesha kesi kama hiyo chini ya mazingira magumu kama hayo. "

Licha ya kutokuelezea undani wa sababu za kujiuzulu, uamuzi huo wa Chanlatte ulifanyika siku moja tu baada ya mmoja wa wasaidizi wake, Ernest Lafortune, kufa katika mazingira ya kutatanisha.

Wadadisi wanasema uamuzi wa jaji Mathieu Chanlatte utachelewesha kesi hiyo inayongojewa kwa hamu kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.