Pata taarifa kuu
HAITI-USALAMA

Haiti: Shughuli mbalimbali zazorota kufuatia uhaba wa mafuta

Ukosefu wa usalama ambao umeathiri Haiti kwa miezi kadhaa unazidisha mgogoro mbaya wa kijamii na kiuchumi ambao unaikumba nchi hiyo.

Mtu huyu anauza madumu karibu na kituo cha mafuta huko Port-au-Prince, Agosti 29, 2019.
Mtu huyu anauza madumu karibu na kituo cha mafuta huko Port-au-Prince, Agosti 29, 2019. AFP - CHANDAN KHANNA
Matangazo ya kibiashara

Vita kati ya makundi hasimu yanayofanya biashara ya dawa za kelevya vinazuia upatikanaji wa vituo vikuu vya mafuta, na kusababisha uhaba wa mafuta kote nchini.

Mitaa ya Port-au-Prince bado imejaa msongamano wa magari lakini wakaazi wanaanza kufikiria jinsi ya kuboresha shughuli kwa sababu, vituo vingi vya gesi vimefungwa.

"Ni kutokana na ukosefu wa usalama unaosababishwa na makundi hasimu. Makundi yanayopatikana kwenye viunga vya Martissant yanazuia usafirishaji wa mafuta kwenye kituo cha Trista. Hii ndio sababisha maeneo yote kukosa kupata mafuta kwa wakati, "amesema Marc Antoine Nesi wa Chama cha Wamiliki wa vituo vya mafuta (Anapross).

Uhaba huu wa mafuta una athari ya moja kwa moja inayotia wasiwasi kwa maisha ya kila siku ya Wahaiti amesema Samendina Lumane Jean wa muungano wa mashirika yanayotetea haki za bnadamu, Défenseurs plus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.