Pata taarifa kuu
HAITI

Haiti: Raia wasubiri misaada ya kimataifa iliyotumwa kwa helikopta

Zaidi ya wiki moja baada ya tetemeko la ardhi nchini Haiti, viongozi walitangaza mwishoni mwa wiki kwamba msaada sasa utawafikia wale walioathiriwa. Kumetumiwa helikopta ili kuweza kusafirisha misaada hiyo, afisa mmoja wa Haiti amesema.

Watu wakipewa chakula huko Les Cayes baada ya tetemeko la ardhi lililotokea Haiti, Agosti 14, 2021.
Watu wakipewa chakula huko Les Cayes baada ya tetemeko la ardhi lililotokea Haiti, Agosti 14, 2021. AFP - REGINALD LOUISSAINT JR
Matangazo ya kibiashara

Kutumia helikopta kwa kusafirisha misaada hiyo kunazuia uporaji kwa misaad inayosafirishwa nhia ya ardhini husuna malori na hasa misaada hiyo walengwa walio katika vijiji ambako ni vigumu kufika.

Kwa kusubiri hadi misaada ya kimataifa ifike, wakaazi kutoka maeneo mengi wanajaribu kujipanga. Baada ya tetemeko la ardhi la Agosti 14, Alex Maxcia, meya wa Corail katika kaunti ya Grand'Anse, alianzisha kile alichokiita "vituo vya mapokezi": "Kuna shule, ofisi na familia za wenyeji. Vituo hivi lazima viheshimu zaidi viwango vinavyotakiwa. "

Ni majengo ambayo yalinusurika kimbunga bila uharibifu mkubwa. Julie Gerthy alikimbilia katika moja ya maeneo haya, kituo cha Msalaba Mwekundu huko Corail. Baada ya nyumba yake kuharibiwa, aliogopa kulala nje: “Tuko salama hapa. Kulala katikati mwa jiji tena barabarani ni hatari sana. Kuna wazururaji. "

Tuko watu wengi wetu hapa. Tunashikamana kwa kusaidiana. Tunajipanga kadiri tuwezavyo. Kwa mfano, ninaweza kuleta chakula kichache, na mwanamke huyu ataleta kitu kingine. Sisi ni kama familia. Tunasaidiana.

Kulingana na meya wa Corail, kati ya wakazi 20,000 wa mji huo, 10,000 sasa wanapatikana katika sehemu hizi za mapokezi katika mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.