Pata taarifa kuu
HAITI-HAKI

Mauaji ya Rais wa Haiti Jovenel Moïse: mshukiwa akamatwa Uturuki

Zaidi ya miezi minne baada ya kuuawa kwa rais Moïse, mahakama ya Haiti inaendelea kusikiliza mashahidi na watu wanaodaiwa kuwa katika kundi lenye silaha lililohusika katika mauaji ya raisa wa Haiti, Jovenel Moïse.

Jovenel Moïse aliuawa usiku wa Julai 6 hadi 7, 2021, katika makazi yake ya kibinafsi. Rais wa Haiti alikuwa na umri wa miaka 53.
Jovenel Moïse aliuawa usiku wa Julai 6 hadi 7, 2021, katika makazi yake ya kibinafsi. Rais wa Haiti alikuwa na umri wa miaka 53. REUTERS/Andres Martinez Casares
Matangazo ya kibiashara

Wafadhili na sababu ya uhalifu huu bado haijulikani, lakini kesi inaendelea. Kama ushahidi, mshukiwa amekamatwa hivi punde nchini Uturuki.

Samir Handal alikamatwa alipowasili katika uwanja wa ndege wa Istanbul ambapo alitarajia kuendelea  hadi Jordan kama hatua ya safari yake ya mwisho. Kwa mujibu wa shirika la habari la Uturuki la DHA, alikuwa akisafiri akiwa na hati za kusafiria za Haiti na Jordan pamoja na pasipoti ya Mamlaka ya Palestina.

Baada ya kuuawa kwa rais Jovenel Moïse Julai 7, polisi ya Haiti ilikuwa imetoa waranti wa kukamatwa dhidi yake kwa "mauaji, jaribio la mauaji na wizi wa kutumia silaha", ikibainisha kuwa mtu huyo anachukuliwa kuwa "hatari na mwenye silaha".

Samir Handal alikamatwa kwenye umbali wa zaidi ya kilomita 9,000 kutoka Port-au-Prince ambapo kulitokea mauaji ya rais Jovenel Moïse. Lakini kukamatwa huku kunazua maswali: wengi wanajiuliza hasa jinsi alivyoweza kupanda ndege ya shirika la kibiashara huko Miami bila kukamatwa.

Sasa kuna pia suala la kukabidhiwa mshukiwa mamlaka husika. Mshukiwa wa kundi la watu waliomuua Jovenel Moïse alikamatwa nchini Jamaica mwezi uliopita, lakini bila makubaliano kuhusu suala hilo na Haiti, inasemekana yuko mbioni kurejeshwa Colombia, nchi yake ya asili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.