Pata taarifa kuu
HAITI-USALAMA

Haiti: Mateka 17 wa kigeni watishiwa kuuawa na kiongozi wa genge lenye silaha

Ukosefu wa usalama unaosababishwa na magenge yenye silaha nchini Haïti unazidi kuitumbukiza nchi hiyo kwenye machafuko ya kila siku.

Kulingana na chanzo cha usalama, watekaji nyara wamedai raia wa Amerika ya Kaskazini fidia ya dola Milioni moja.
Kulingana na chanzo cha usalama, watekaji nyara wamedai raia wa Amerika ya Kaskazini fidia ya dola Milioni moja. Richard PIERRIN AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi hii tayari imerekodi zaidi ya visa 119 vya utekaji nyara tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, visa ambavyo ni zaidi ya vile vilivyorekodiwa kwa mwezi mzima wa Septemba. Kuongezeka kwa visa hivi vya utekaji nyara kunakuja wakati kiongozi wa genge lililowateka nyara raia 17 kutoka Amerika ya Kaskazini Jumamosi (Oktoba 16) anatishia kuwaua leo Ijumaa.

Video iliyorekodiwa ilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii Alhamisi, Oktoba 21, lakini tukio hilo lilikokea Jumatano. Mbele ya majeneza ambayo zilikuemo maiti za watu watano katiya wapiganaji wake, waliuawa na polisi, Wilson Joseph, kiongozi wa genge hilo linaloitwa "400 mawozo" amesema kwamba ikiwa " "hatapati kile anachohitaji, atawaua Wamarekani anaowashikilia".

Fidia kubwa mno

Ni siku ya sita tangu kundi la wamishonari na watu wa familia zao walipotekwa nyara katika eneo linalodhibitiwa na genge hili lenye silaha. Raia 16 wa Marekani na raia mmoja wa Canada, wakiwemo watoto watano, mdogo wao akiwa na miezi nane tu. Kulingana na chanzo cha usalama, watekaji nyara wa raia hawa wa Amerika Kaskazini wamedai dola milioni moja kama fidia kwa kila mtu.

Makundi, ambayo yamekuwa yakiongeza visa vya utekaji nyara tangu msimu huu wa joto na ambayo Wahaiti ndio waathiriwa wa kwanza, hawasiti kudai ukombozi kama huo wa makumi, mamia ya maelfu ya dola, hata kama familia za mateka wao zinaishi wanakabiliwa na umaskini mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.