Pata taarifa kuu
HAITI-USALAMA

Ukosefu wa usalama Haiti: Mgomo na mazungumzo ya kuwaachilia mateka 17 vyaendelea

Wakazi wengi wa miji na hasa mji mkuu wa Haïti, Port-au-Prince walibaki nyumbani Jumanne Oktoba 19, bado wakifuata wito wa mgomo uliotolewa wiki iliyopita na vyama kadhaa vya wafanyakazi kupinga dhidi ya ukosefu wa usalama.

Siku ya mgomo wa jumla huko Port-au-Prince, Haiti, Jumatatu, Oktoba 18, 2021.
Siku ya mgomo wa jumla huko Port-au-Prince, Haiti, Jumatatu, Oktoba 18, 2021. AP - Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Kisa cha utekaji nyara Jumamosi, Oktoba 16 cha raia 17 kutoka Amerika Kaskazini kilichotekelezwa na moja ya magenge yenye nguvu zaidi nchini Haïti kilioneza shinikizo kwa wito huu.

Shule na ofisi za serikali bado zilifungwa Jumanne wiki hii katika mji mkuu lakini, ikilinganishwa na Jumatatu, mgomo huo umepunguza kasi na shughuli mbalimbali kwenye barabara kuu za mji mkuu Port-au-Prince.

Maduka ya dawa na maduka makubwa yalifunguliwa siku nzima katika baadhi ya maeneo ya mki mkuu. Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wameebaini kwenye vyombo vya habari nchini Haïti kwamba kiuchumi hawawezi kufunga shughuli zao kutokana na hali ya maisha inayowakabili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.