Pata taarifa kuu
HAITI-USALAMA

Haiti: Utawala wa Biden wasalia kimya kuhusu utekaji nyara wa Wamarekani 16

Bado hakuna habari ya Wamarekani kumi na sita na Wakanada waliotekwa nyara Jumamosi, Oktoba 16 nchini Haiti na genge lenye silaha ambalo pia liliwateka raia wengi wa Haïti.

Wamarekani kumi na sita na raia mmoja wa Canada walitekwa nyara nchini Haiti, Jumamosi, Oktoba 16, baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima cha Maison La Providence de Dieu huko Croix-des-Bouquets.
Wamarekani kumi na sita na raia mmoja wa Canada walitekwa nyara nchini Haiti, Jumamosi, Oktoba 16, baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima cha Maison La Providence de Dieu huko Croix-des-Bouquets. © Odelyn Joseph/AP
Matangazo ya kibiashara

Kundi la raia wa Marekani lilikuwa liimetembelea kituo cha watoto yatima katika moja ya maeneo hatari zaidi nchini humo. Mamlaka nchini Marekani haijachukulia rasmi utekaji nyara huu wa uliowashangaza wengi. Lakini habari hii imegonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari vya Marekani.

Hakuna habari rasmi juu ya mazungumzo yoyote yanayoendelea na watekaji nyara wa Wamarekani kumi na sita na raia mmoja wa Canada. Lakini Gazeti l Miami Herald linaripoti kwamba maafisa wa FBI kutoka Marekani wamewasili katika mji mkuu wa Haïti, Port-au-Prince.

Wakati utawala wa Biden umesalia kimya ili usihatarishe maisha ya mateka hao, Adam Kinzinger, mjumbe wa Kamati ya Mambo ya nje ya Baraza la Wawakilishi la Marekani, alizungumza kwenye kituo cha CNN Jumapili (Oktoba 17). Mbunge huyo kutoka chama cha Republican alihakikishia kwamba Marekani itafanya kilio chini ya uwezo wake ili kuwakomboa wamishonari na familia zao. Lakini pia alisema hakukuwa na swali la kulipa fidia na kwamba, ikiwa ni lazima, "jeshi au polisi litatumiwa" ili kuokoa mateka hao.

Shambulio la genge dhidi ya Waziri Mkuu

Jarida la New York Times linasema kuwa wageni, hasa Wamarekani, wamekuwa wakilengwa na magenge yenye silaha nchini Haiti ambao wanaona kama kuna uwezekano wa kuomba fidia kubwa. Kisa hiki cha utekaji nyara kinaleta changamoto mpya kwa serikali ya mpito ya Haiti. Siku ya Jumapili, Kaimu Waziri Mkuu Ariel Henry alilazimika kukimbia akikabiliwa na risasi nzito katika kitongoji cha Port-au-Prince kinachodhibitiwa na magenge yenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.