Pata taarifa kuu
HAITI-SIASA

Haiti: Mvutano wajitokeza kati ya China na Marekani juu ya mustakabali wa ushiriki wa UN

Mustakabali wa ujumbe wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, ambao muda wake wa kuhudumu nchini humo unakamilika Ijumaa hii jioni, Oktoba 15, umekumbwa na mvutano mkali huko New York kati ya wajumbe wa umoja huo.

Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi, Oktoba 14 uliambulia patupu kuhusiana na kuongezwa kwa muda wa ujumbe wa umoja wa Mataifa kuendelea kuhudumu nchini Haïti.
Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi, Oktoba 14 uliambulia patupu kuhusiana na kuongezwa kwa muda wa ujumbe wa umoja wa Mataifa kuendelea kuhudumu nchini Haïti. TIMOTHY A. CLARY AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao walikutana Alhamisi wiki hii walishindwa kuafikia kuhusu kuongezea muda ujumbe huo kuendelea kuhudumu nchini Haiti, kwani wanadiplomasia hawakukubaliana juu ya maelezo ya nakala ya azimio hilo.

Marekani, ambayo kwa inashughulikia kesi ya Haiti katika Umoja wa Mataifa, ilipendekeza kuongezea upya kipindi cha mwaka mmoja ujumbe wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa, lakini China ilifutilia mbali pendekezo hilo.

China imeivalia njuga Haiti.Tangu Haiti itambue rasmi Taiwan kama taifa huru, Beijing imetumia ushawishi wake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vizuizi katika masuala yanayoihusu. Mwezi Juni mwaka huu, China ilifutilia mbali rasimu ya tamko la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kusikitishwa na kuzorota kwa hali ya usalama nchini Haiti, kabla tu ya mauaji ya rais Jovenel Moïse.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.