Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Haiti: Zaidi ya wahalifu 250 waliuawa na watu wanaojiita walinzi tangu Aprili

Watu 264 wanaoshukiwa kuwa katika makundu ya wahalifu wameripotiwa kuuawa na wakazi wa visiwani humo walioamua kuchukua sheria mkononi.

Antonio Guterres akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Port-au-Prince mnamo Julai 1, 2023, wakati wa ziara ya mshikamano katika kisiwa kilichokumbwa na migogoro.
Antonio Guterres akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Port-au-Prince mnamo Julai 1, 2023, wakati wa ziara ya mshikamano katika kisiwa kilichokumbwa na migogoro. REUTERS - RALPH TEDY EROL
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu 264 wanaoshukiwa kuwa katika makundi haya ya wahalifu wameuawa nchini Haiti tangu mwezi Aprili, na waliuawa na watu wanaojiita walinzi. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwenye tovuti alitoa maoni juu ya takwimu hizi, akionyesha wasiwasi kuhusu tukio hili katika nchi hii iliyokumbwa na migogoro ya kijamii na kiuchumi.

"Kuibuka kwa makundi ya watu wanaojitangaza kuwa walinzi waliojitolea kunaongeza kiwango kipya cha uhasama. Tangu mwezi Aprili, Binuh (Ofisi Jumuishi ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti) imehesabu angalau watu 264 wanaodaiwa kuwa wanachama wa magenge waliouawa na makundi ya watu waliojitangaza kuwa walinzi,” María Isabel Salvador ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

'Hali mbaya ya kibinadamu'

Kutokana na kushindwa kwa polisi kukabiliana na ghasia ambazo hazijawahi kushuhudiwa za magenge ambayo yanadhibiti sehemu kubwa ya eneo la mji mkuu Port-au-Prince, wakaazi wameamua kuchukua sheria mikononi, wakati jumuiya ya kimataifa bado haijapata nchi ya kuongoza kikosi cha kuingilia kati kilichoombwa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Haiti.

"Watu wa Haiti wamenaswa katika jinamizi la mauaji," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema siku ya Alhamisi. "Hali ya kibinadamu ni zaidi ya ya kutisha. Magenge katili yana udhibiti wa raia wa Haiti,” aliongeza.

Na "hakuwezi kuwa na suluhu la kudumu na shirikishi la kisiasa bila ya uboreshaji mkubwa katika hali ya usalama," alisisitiza katibu mkuu, akirudia wito wake wa kutuma kikosi cha kimataifa kusaidia polisi na "kusambaratisha" magenge hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.