Magenge yenye silaha kero nchini Haiti
NAIROBI – Ukosefu wa usalama katika mji mkuu wa Haiti umefikia viwango sawa na nchi zilizo kwenye vita, umoja wa mataifa ulisema Jumatatu katika ripoti iliyoangazia kuongezeka kwa mauaji na utekaji nyara wa watu nchini humo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Magenge yenye silaha "yameedelela kushindana ili kupanua udhibiti wa eneo lao katika eneo lote la mji mkuu wa Port-au-Prince, na kuenea katika vitongoji ambavyo havijaathiriwa hapo awali," ilisema ripoti hiyo, kutoka kwa Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres.
"Pamoja na idadi kubwa ya vifo na kuongezeka kwa maeneo chini ya udhibiti wa magenge yenye silaha, ukosefu wa usalama katika mji mkuu umefikia viwango sawa na nchi zilizo katika vita vya silaha," ilieleza zaidi ripoti hiyo ya UN.
"Watu wa Haiti wanaendelea kukumbwa na mojawapo ya mizozo mibaya zaidi ya haki za binadamu katika miongo kadhaa na dharura kubwa ya kibinadamu," ripoti hiyo ilisema.
Kati ya Aprili 14 na 19, mapigano kati ya magenge hasimu yalisababisha vifo vya karibu watu 70, wakiwemo wanawake 18 na angalau watoto wawili, taarifa hiyo iliongeza.
Guterres mwezi Oktoba alitoa mwito wa kuomba msaada kutoka kwa waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry, akiomba baraza la usalama kutuma msaada kusaidia polisi kurejesha utulivu.