Pata taarifa kuu

Antonio Guterres atoa wito wa msaada nchini Haiti, inayokumbwa na makundi ya wahalifu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alikutana na Waziri Mkuu Ariel Henry na wajumbe wa Baraza la Mpito, wanasiasa na mashirika ya kiraia wakati wa ziara yake nchini Haiti siku ya Jumamosi. Mazungumzo mazuri yalifanyika, kulingana na Antonio Guterres, kuhusu mzozo mkubwa ambao umekuwa ukiendelea nchini kwa muda.

Antonio Guterres akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Port-au-Prince mnamo Julai 1, 2023, wakati wa ziara ya mshikamano katika kisiwa kilichokumbwa na shida.
Antonio Guterres akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Port-au-Prince mnamo Julai 1, 2023, wakati wa ziara ya mshikamano katika kisiwa kilichokumbwa na shida. REUTERS - RALPH TEDY EROL
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Port-au-Prince, Marie-André Bélange

Ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ilichukua saa chache. Kana kwamba ni kutoa nafasi kwa mshikamano huu anaokuja kuzungumzia kwa raia wa Haiti, Antonio Guterres alianza kw kuzungumza kwa lugha ya Krioli (lugha iliyozaliwa nchini Haiti) wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa kidiplomasia wa uwanja wa ndege.

"Vita vya magenge vimezidisha mazingira magumu ya Wahaiti. Hali nchini Haiti inatia wasiwasi,” amebainisha Antonio Guterres. “Mmoja kati ya watu wawili nchini Haiti anaishi katika umaskini uliokithiri na anakabiliwa na njaa, bila kupata maji ya kunywa mara kwa mara. »

Kunahitajika msaada

Haiti haiwezi kuondokana na shida hizi yenyewe, inahitaji msaada. Mjini Port-au-Prince, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitoa wito wake kwa jumuiya ya kimataifa. “Ninaendelea kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha kutumwa mara moja kwa kikosi cha usalama cha kimataifa ili kusaidia Polisi wa Haiti katika vita dhidi ya magenge. "

Ni juu ya Wahaiti kutafuta suluhu ya mgogoro huo, pia amesisitiza. Makubaliano ya kisiasa yanahitajika kumaliza mzozo huo. Kupinduliwa kwa masilahi ya kibinafsi, makubaliano na maono ya pamoja, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametetea kufikia lengo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.