Pata taarifa kuu

Haiti : Watu zaidi elfu mbili wameuawa tangu kuanza kwa machafuko mwaka huu

Nairobi – Watu zaidi ya 2,400 wameuwa nchini Haiti tangu kuanza kwa mwaka huu, wakati huu magenge yenye silaha yakiendelea kusababisha utovu wa usalama hasa katika jiji kuu la Port-au-Prince.

Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakikabiliana na maofisa wa polisi nchini Haiti
Magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yakikabiliana na maofisa wa polisi nchini Haiti © AFP/Richard Pierrin
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa kwenye ripoti yake inasema, wiki hii pekee, watu zaidi ya 30 wameuawa jijini Port-au-Prince na mamia kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na makundi hayo yenye silaha.

Hata hivyo, kati ya Januari 1 hadi Agosti 15 mwaka huu, watu 2,439 wameuawa na wengine 902 wamejeruhiwa, huku wengine 951 wakitekwa.

Kuendelea kwa mauaji haya, kunaendelea kuzua wasiwasi na hasira miongoni mwa raia ambao wameunda vikundi vya kujilinda, suala ambalo Umoja wa Mataifa, unaonya kuwa unaendelea kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.

Mbali na visa vya mauaji na utekaji, makundi yenye silaha yanateka magari, kuiba mali ya watu na kuwabaka wanawake na wasichana, hali ambayo imesababisha watu zaidi ya Elfu tano kuukimbia mojawapo wa mataa wa jiji la Port-au-Prince.

Tangu kuuliwa kwa rais Jovenel Moise mwaka 2021, hali ya usalama nchini Haiti imeendelea kuwa mbaya na Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, unaomba hatua ya haraka kuchukuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.