Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Mexico: Wanawake wawili kugombea kiti cha urais mwaka wa 2024

Wanawake wawili watawania kiti cha urais kwa mara ya kwanza mwaka 2024 nchini Mexico, ambapo meya wa zamani wa Jiji la Mexico Claudia Sheinbaum aliteuliwa Jumatano kuwa mgombea wa chama tawala, Movement for National Regeneration (MORENA, kushoto).

Xochitl Galvez (kushoto) na Claudia Sheinbaum (kulia) wote ni wagombea wa kiti cha urais nchini Mexico.
Xochitl Galvez (kushoto) na Claudia Sheinbaum (kulia) wote ni wagombea wa kiti cha urais nchini Mexico. © Henry Romero & Daniel Becerril, Reuters - Montage FMM
Matangazo ya kibiashara

Bi Sheinbaum, 61, atakuwa na mpinzani wake mkuu Seneta Xochitl Galvez, 60, ambaye aliteuliwa kuwa mgombea Jumapili baada ya kutawala kura za mchujo za muungano unaoleta pamoja vyama vitatu vya upinzani.

Kwa hivyo mwanamke ana nafasi kubwa ya kumrithi rais anayemaliza muda wake Andres Manuel Lopez Obrador mnamo 2024 kama rais wa Mexico, nchi ya pili kwa uchumi mkubwa katika Amerika ya Kusini unaoelekezwa kuelekea Marekani.

Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii ambayo inarekodi maelfu ya mauaji ya wanawake kwa mwaka, pamoja na vurugu kubwa ya magendo ya madawa ya kulevya katika baadhi ya maeneo ya nchi hii.

Mwanasayansi kwa mafunzo, aliye karibu na rais anayemaliza muda wake, Bi.Sheinbaum alichukuwa nafasi ya kwanza katika uchunguzi wa maoni ulioandaliwa na chama chake cha MORENA kati ya jumla ya wagombea sita.

Akiwa amechochewa na umaarufu wa rais anayemaliza muda wake, kwa sasa ndiye anayependwa zaidi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mapema mwezi Juni.

"Leo ni watu wa Mexico ambao wameamua," amesema baada ya kutangazwa kwa matokeo. "Mchakato wa uchaguzi unaanza kesho katika ngazi ya kitaifa. Hakuna dakika ya kupoteza."

Hata kabla ya matokeo kutangazwa, mpinzani mkuu wa Bi Sheinbaum, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Marcelo Ebrard, alidai marudio ya kura hiyo ya maoni, akikashifu “ukiukwaji wa sheria”.

Akiwa peke yake kati ya wagombea sita, Bw. Ebrard alipuuza kutangazwa kwa matokeo hayo, akidai kuwa mmoja wa wawakilishi wake alipigwa na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.