Pata taarifa kuu

Mexico: Mwandishi wa habari auawa, wa pili ndani ya kipindi cha wiki moja

Mwandishi wa habari wa Mexico aliuawa kwa kupigwa risasi Jumamosi Julai 15 huko Acapulco (magharibi), wa pili ndani ya kipindi cha wiki moja nchini Mexico, mojawapo ya nchi hatari zaidi duniani kwa waandishi wa habari kutokana na ghasia za uhalifu uliopangwa.

Wanajeshi wa jeshi la Mexico na maafisa wa polisi wa serikali katika eneo ambalo mwandishi wa habari wa Mexico Nelson Matus aliuawa katika mji wa mapumziko wa Acapulco, katika jimbo la Guerrero, Mexico, Julai 15, 2023.
Wanajeshi wa jeshi la Mexico na maafisa wa polisi wa serikali katika eneo ambalo mwandishi wa habari wa Mexico Nelson Matus aliuawa katika mji wa mapumziko wa Acapulco, katika jimbo la Guerrero, Mexico, Julai 15, 2023. AFP - FRANCISCO ROBLES
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa tovuti ya habari nchini humo, Nelson Matus aliuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la maegesho karibu na duka la bei nafuu, imebaini ofisi ya mwendesha mashitaka wa eneo hilo, ambayo imetangaza kufunguliwa kwa uchunguzi wa "uhalifu wa mauaji kwa kutumia silaha", na kuahidi kufanya kinachowezekana kuwapata wahalifu.

Nelson Matus alikuwa na uzoefu wa miaka 15 kama mwandishi wa habari. Alibobea katika kuangazia ghasia zilizochochea jimbo la Guerrero (kusini-magharibi), mjumbe wa shirika lisilo la kiserikali la Reporters Without Borders (RSF), Balbina Flores ameliambia shirika la habari la AFP. 

Tovuti ya habari ya Lo Real de Guerrero ailiyobobea katika mambo mbalimbali, ambayo Bw. Matus alikuwa mkurugenzi wake, kwa mfano ilichapisha makala siku ya Jumamosi kuhusu ugunduzi wa "mabaki ya binadamu kwenye mifuko nyeusi" karibu na hoteli moja huko Acapulco.

Mnamo Julai 8, mwili wa Luis Martin Sanchez ulipatikana ukiwa na majeraha, siku chache baada ya kutoweka kwa mwandishi wa gazeti la kila siku la La Jornada katika jimbo la Nayarit (kaskazini-magharibi). Huku waandishi wa habari 13 wakiuawa kulingana na hesabu ya mamlaka, mwaka 2022 ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa waandishi wa habari nchini Mexico tangu mwaka 2000. Nchi hiyo ni mojawapo ya nchi zenye vurugu zaidi duniani, huku zaidi ya waandishi wa habari 150 wakiuawa tangu mwaka 2000, kulingana na RSF.

Shirika lisilo la kiserikali la Mexico Kifungu cha 19 limeorodhesha kwa upande wake tangu 2000 "visa 160 vya mauaji ya waandishi wa habari nchini Mexico, kuhusiana na uwezekano wa kazi yao" ya uandishi wa habari.

'Guerrero inapitia hali ngumu sana'

Jimbo lililoathiriwa zaidi ni Veracruz (kusini mashariki), na visa 31 vya mauaji ​​ya waandishi wa habari tangu 2000, hasa katika miaka ya 2010, kulingana na RSF. Guerrero inashika nafasi ya pili kwa visa 15 vya mauaji ya waandishi wa habari tangu 2000 (dhidi ya visa viwili ya mauaji katika mji mkuu wa Mexico). Guerrero ni mojawapo ya majimbo yaliyoathiriwa zaidi na madai ya ghasia zinazohusiana na dawa za kulevya.

"Guerrero inapitia hali ngumu sana. Inakabiliwa na viwango vya juu sana vya ghasia, jambo ambalo linawafanya waandishi wa habari kuwa hatarini zaidi, hasa wale wanaoandika habari,” kulingana na mjumbe wa RSF Balbina Flores.

Siku ya Jumatatu, waandamanaji waliuzingira mji mkuu wa jimbo, Chilpancingo: Wanajeshi 13 wa vikosi vya usalama na watumishi wa umma walichukuliwa mateka, mlango wa jumba la gavana ulivunjwa na gari la kivita lililoibiwa kutoka kwa polisi, barabara kuu imefungwa... watumishi waliachiliwa hatimaye baada ya mazungumzo kati ya serikali ya shirikisho na waandamanaji, ambao waliaminika kuwa waliingiliwa na uhalifu uliopangwa, mamlaka ilisema.

Mauaji mengi ya waandishi wa habari hayaadhibiwi, RSF inasikitika. Siku ya Jumatatu, waandishi wa habari kadhaa walikusanyika katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na Mexico, kupinga mauaji ya mwandishi wa Gazeti laJornada.

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Mexico imetoa wito wa uchunguzi wa "haraka, wa kina, huru na wenye ufanisi" kulaani mauaji ya Bw. Sanchez.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.