Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Mexico: Uchaguzi wafanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa urais

Mamilioni ya wananchi wa Mexico wameanza kupiga kura siku ya Jumapili katika jimbo lenye watu wengi zaidi nchini humo, ambapo chama tawala la mrengo wa kushoto cha Morena kinaweza kuimarisha ushawishi wake kwa kuteka ngome kuu ya mwisho ya chama kikuu cha zamani cha PRI kinachoongoza, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa rais.

Mji wa Mexico.
Mji wa Mexico. © Fernando Espinosa de los Monteros / GettyImages
Matangazo ya kibiashara

Jumla ya wapiga kura milioni 12.6 watamchagua gavana wa Jimbo la Mexico, eneo lililo nje kidogo ya mji mkuu ambalo linajumuisha tofauti zote za Mexico, kati ya vurugu na mabadiliko ya kiuchumi.

Katika jaribio hili kubwa la mwisho kabla ya uchaguzi wa urais wa katikati ya mwaka 2024, mgombea wa chama tawala cha Morena Delfina Gomez ndiye anayependekezwa zaidi dhidi ya mgombea wa chama cha PRI Alejandra del Moral.

Ushindi wake mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa urais utathibitisha enzi mpya ya chama cha Morena, ambacho kinatawala majimbo 22 kati ya 32 ya shirikisho hilo, pekee au na washirika wake.

Delfina Gomez anasukumwa na umaarufu wa Rais Andres Manuel Lopez Obrador, madarakani tangu Desemba 2018.

Madarakani kutoka 1930 hadi 2000, kurudi tena madarakani kati ya 2012 na 2018, Chama cha Mapinduzi cha PRI, kilielezea wakati wake kama "udikteta kamili" wa mshindi wa Tuzo ya Nobel Mario Vargas Llosa, kwa hivyo kitapoteza ngome yake ya kihistoria ya uchaguzi.

"Natumai itakuwa siku nzuri kwa watu wa Mexico, walio na utulivu," amesema Delfina Gomez wakati akipiga kura.

Likiwa na wakazi milioni 17 - sawa kama Uholanzi, zaidi ya Quebec au Ubelgiji - Jimbo la Mexico ni "Jamhuri ndogo ya Mexico", kulingana na mwanasayansi wa siasa Miguel Tovar wa kampuni ya Alterpraxis.

Jimbo hilo linakumbwa na vurugu zaidi nchini, hasa katika miji ya mkusanyiko wa mji mkuu (Ecatepec, nk). Uchumi wake unawakilisha 9.1% ya Pato la Taifa.

Uchaguzi pia unafanyika Jumapili katika jimbo la madini la Coahuila (kaskazini).

Katika jimbo hili linalopakana na Marekani, chama cha Morena kimejikuta kikiwa na wagombea wawili, ikiwa ni pamoja na kugombea kwa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya Lopez Obrador.

Mgawanyiko wa chama kilicho madarakani unaweza kuwezesha chama cha PRI kinashikilia wingi wa kura kwa wapiga kura milioni 2.3 waliojiandikisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.