Pata taarifa kuu

Takriban watu 15 wafariki katika ajali ya barabarani nchini Mexico

Takriban watu kumi na watano walifariki dunia siku ya Ijumaa nchini Mexico katika ajali ya basi la watalii lililopinduka barabarani katika jimbo la Nayarit (magharibi), imetangaza mamlaka ya eneo hilo.

Maafisa wa Polisi wa Mexico.
Maafisa wa Polisi wa Mexico. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Katika hatua hii watu kumi na watano wamefariki", ikiwa ni pamoja na watoto wawili, na wengine wengi kujeruhiwa, imesema Wizara ya Usalama katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Waathiriwa ni watalii kutoka jimbo la Guanajuato (katikati) ambao walikuwa wakirejea León, jiji kubwa zaidi katika jimbo hili, baada ya likizo.

Kanda za video zilizotolewa na mamlaka kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha basi hilo likipinduka kwenye bonde lisilo na kina kando ya barabara.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, basi hilo lilikuwa limebeba abiria 48, madereva wa teksi na familia zao ambao walikuwa wamepanga safari hii ya mwisho wa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.