Pata taarifa kuu

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Peru na Mexico watokota

Siku ya Jumanne, Peru ilimtangaza balozi wa Mexico kuwa mtu asiyestahili na kuomba aondoke kwenye ardhi yake. Balozi Mexico alitoa hifadhi ya kisiasa kwa familia ya rais wa zamani wa Peru, Pedro Castillo, aliyeachishwa madaraka mapema Desemba.

Hatima ya Rais wa zamani wa Peru Pedro Castillo, pichani hapa tarehe 7 Desemba 2021, iko hatarini.
Hatima ya Rais wa zamani wa Peru Pedro Castillo, pichani hapa tarehe 7 Desemba 2021, iko hatarini. AFP - CARLOS MAMANI
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Mexico ametangazwa kuwa mtu asiyefaa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Peru César Landa alitangaza siku ya Jumanne, Desemba 20, 2022. Aliongeza kuwa mwanadiplomasia huyo ana saa sabini na mbili kuondoka katika ardhi ya Peru. Nchi hizo mbili zinakiingana katika mzozo wa kidiplomasia baada ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa Rais wa Peru Pedro Castillo. Tangazo la kufukuzwa linakuja baada ya balozi wa Mexico kutoa hifadhi ya kisiasa kwa familia yake ya Pedro Castillo.

Kwa upande wake, kiongozi wa Mexico Andrés Manuel Lopez Obrador alisema yuko tayari kutoa hifadhi kwa rais huyo wa zamani baada ya kufutwa kazi. Alisisitiza kumuunga mkono Pedro Castillo kwa kukataa kutambua utawala wa rais mpya wa Peru, Dina Boluarte.

Familia ya Pedro Castillo na Balozi wa Mexico wameondoka kwenye Ubalozi wa Mexico huko Lima, Peru. Kwa upande wake, Pedro Castillo bado amefungwa. Jamaa huyo alikamatwa na jeshi kwa "uasi" na "njama" baada ya kujaribu mapinduzi mnamo Desemba 7 mbele ya uhasama kutoka kwa Bunge.

Peru ilimpa balozi huyo siku tatu kuondoka nchini humo. Kufukuzwa "kusiko na haki na ni hatu ya kulaumiwa" kulingana na mkuu wa diplomasia ya Mexico. Hata hivyo, Mexico  inaamini katika mazungumzo na inahakikisha kwamba uwakilishi wake wa kidiplomasia utaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.