Pata taarifa kuu

Peru: Rais atangaza kurejesha nyuma uchaguzi mkuu baada ya maandamano yenye ghasia

Katika ujumbe uliorushwa na televisheni usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, Dina Boularte alitangaza kwamba atawasilisha muswada unaolenga kurejsha nyuma uchaguzi mkuu kutoka mwaka 2026 hadi mwezi Aprili 2024 wakati nchi ikikumbwa na maandamano ambayo yamesababisha vifo vya watu wawilileo mchana, baada ya rais Pedro Castillo kutimuliwa mamlakani, wiki moja iliyopita.

Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Pedro Castillo nje ya Bunge la Congress mjini Lima, Jumapili, Desemba 11, 2022.
Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Pedro Castillo nje ya Bunge la Congress mjini Lima, Jumapili, Desemba 11, 2022. AP - Martin Mejia
Matangazo ya kibiashara

Siku chache zilizopita, baada tu ya kuachishwa kazi na kukamatwa kwa Pedro Castillo, Dina Boluarte alisema nia yake ni kuendeleza mamlaka yake hadi mwezi Julai 2026. Lakini maandamano tayari yameibuka na kutaka uchaguzi ufanyike haraka. Na uundaji, Jumamosi, wa serikali yenye wasifu huru na wa kiufundi hautabadilisha chochote.

Akisema kuelewa "nia ya raia", Dina Boluarte, makamu wa rais hadi kuapishwa kwake Desemba 7, alisema katika ujumbe wa televisheni jana usiku kwamba "ameamua kuchukua hatua ya makubaliano (...) ili kufupiza uchaguzi mkuu hadi mwezi Aprili 2024”, baada ya mzozo uliosababishwa na jaribio lisilofanikiwa la Pedro Castillo kulivunja Bunge.

Hali ya dharura

Dina Boluarte pia alitoa tangazo la hali ya hatari katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na maandamano. "Nilitoa maagizo ya kurejesha udhibiti wa utaratibu wa ndani na haki za msingi za raia," alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.