Rais mpya wa Peru awataka wananchi kumpa muda wa kurosha kutokomeza rushwa
Nchini Peru, rais mpya Dina Boluarte ameanza kupata shinikizo za kuunda serikali, siku moja baada ya kuapishwa katika nafasi hiyo, kufuatia kuondolewa madarakani na kukamatwa kwa mtangulizi wake Pedro Castillo, baada ya jaribio la kulivunja bunge na kutaka kutawala kwa mkono wa chuma.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matangazo ya kibiashara
Baada ya kuapishwa kuongoza taifa hilo la America Kusini, katika kipindi hiki cha mvutano mzito wa kisiasa, ameomba, muda ili kupambana na ufisadi na kuimarisha uongozi wa nchi hiyo.
Ninachokiomba ni kupewa muda ili nipambane na rushwa na kuliokoa taifa letu kutokana na uongozi mbaya.
Rais huyo mpya, anatarajiwa kukaa madarakani, hadi mwezi wa Julai 2026 wakati muhula wa mtangulizi wake, Pedro Castillo, utakapomalizika.