Pata taarifa kuu

Peru: Yenifer Paredes, shemeji wa Rais Castillo ajisalimisha mbele ya vyombo vya sheria

Yenifer Paredes shemeji wa rais wa Peru ambaye amekuwa akitafutwa na vyombo vya sheria nchini humo hata katika majengo ya ikulu ya rais, alijisalimisha kwa hiari Jumatano Agosti 10. Anaweza kuzuiliwa kwa muda wa siku kumi kama sehemu ya uchunguzi wa ufisadi unaomhusisha Pedro Castillo.

Yenifer Paredes, shemeji wa rais wa Peru Pedro Castillo,   alijisalimisha mbele ya vyombo vya usalama mnamo Agosti 11, baada ya msako katika ikulu na makazi ya rais wa jamhuri.
Yenifer Paredes, shemeji wa rais wa Peru Pedro Castillo, alijisalimisha mbele ya vyombo vya usalama mnamo Agosti 11, baada ya msako katika ikulu na makazi ya rais wa jamhuri. AFP - ERNESTO ARIAS
Matangazo ya kibiashara

Yenifer Paredes ambaye amelelewa kama binti ya rais na mkewe, anashutumiwa kwa kufanya biashara ya ushawishi na kosa dhidi ya utawala wa umma. Kulingana na upande wa mashtaka, alitumia fursa ya ukaribu wake na rais Pedro Castillo kushindia zabuni kwa kampuni ambayo amekuwa akifanyia kazi na wamiliki wake walikamatwa Jumanne.

Ujenzi wa mitaro ya kupitishia maji

Yenifer Paredes, hasa, alirekodiwa akitoa soko la ujenzi wa mitaro ya maji taka huko Cajamarca, mkoa anakotoka rais Pedro Castillo. Mnamo mwezi Julai, wakati wa akisikilizwa mbele ya tume ya uchunguzi ya bunge, Yenifer Paredes alijitambulisha kama mfanyakazi wa kawaida asiye na mamlaka ya kweli.

Kwa kushawishika kwamba Paredes hangeweza kuchukua hatua bila rais na mkewe kujua, mwendesha mashtaka amemuagiza hadi kitengo cha polisi chenye mamlaka ya uchunguzi kama sehemu ya hatua ya kumuweka kizuizini kwa siku kumi kabla ya kesi kuanza.

Mpango wa vyombo vya habari

Rais Pedro Castillo ameshutumu kuwepo kwa mpango wa vyombo vya habari kwa lengoa la kumpokonya mamlaka "kinyume cha sheria na kinyume cha katiba". Kulingana na rais huyo, ni mkanganyiko kati ya Bunge la Congress linaloongozwa na upinzani, ambalo limejaribu kumuondoa madarakani mara mbili, na vymbo vya sheria ambavyo vimeanzisha uchunguzi wa ufisadi mara tano dhidi yake na wasaidizi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.