Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Marekani: Mhusika wa shambulio la chuki dhidi ya Wayahudi Pittsburgh ahukumiwa kifo

Mhusika wa shambulio kwa kutumia silaha la mwaka 2018 kwenye sinagogi la Pittsburgh, shambulio baya zaidi dhidi ya Wayahudi katika historia ya Marekani, alihukumiwa kifo na mahakama ya shirikisho siku ya Jumatano, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti. Lakini hukumu hiyo inaweza isitekelezwe, kwa sababu ya kusitishwa kwa adhabu ya kifo nchini Marekani. Jumla ya watu 11 waliuawa katika shambulio hilo.

Nyota ya Daudi yawekwa kwa heshima ya wahanga wa shambulio baya zaidi dhidi ya Wayahudi katika historia ya Marekani, katika Sinagogi la Tree of Life huko Pittsburgh, Julai 13, 2023.
Nyota ya Daudi yawekwa kwa heshima ya wahanga wa shambulio baya zaidi dhidi ya Wayahudi katika historia ya Marekani, katika Sinagogi la Tree of Life huko Pittsburgh, Julai 13, 2023. © Gene J. Puskar / AP
Matangazo ya kibiashara

Majaji katika mahakama ya shirikisho huko Pennsylvania walipiga kura kwa kauli moja Jumatano kumhukumu kifo mtu ambaye aliwaua waumini 11 wa sinagogi la Pittsburgh mwaka wa 2018. Wizara ya sheria ya Marekani ilitangaza kusitishwa kwa hukumu ya kifo, hata hivyo hukumu ya kifo inaweza isitekelezwe dhidi ya mhusika wa shambulio hilo.

Adhabu hii ya kifo ni ya kwanza chini ya rais Joe Biden

Majaji 12 wa mahakama ya shirikisho huko Pennsylvania (kaskazini mashariki) walipiga kura kwa kauli moja kuunga mkono hukumu ya kifo dhidi ya Robert Bowers, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa mwendesha mashtaka Eric Olshan, mwakilishi wa ndani wa wizara ya Sheria ya Marekani.

Wakati wa awamu ya kwanza ya kesi hii ya kipekee ya miezi mitatu - katika muktadha wa kuongezeka kwa vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi na hofu ya kuibuka tena kwa makundi ya Wanazi mamboleo na wazungu wenye msimamo mkali- dereva huyu mwenye umri wa miaka 50 alipatikana na hatia katikati mwa mwezi Juni ya mauaji 11 yaliyokithiri karibu miaka mitano iliyopita katika Sinagogi ya Tree of Life huko Pittsburgh.

Hukumu hii lazima itamkwe rasmi Alhamisi na jaji wa shirikisho, lakini kwa vile Wizara ya Sheria ilitangaza kusitishwa kwa adhabu ya kifo nchini Marekani , huenda adhabu ya kifo isitumike kamwe dhidi ya Robert Bowers.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.