Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Joe Biden ahimiza kukomesha 'janga la vurugu za bunduki'

Rais Joe Biden ametoa wito hivi punde siku ya Jumanne, katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa Marekani, kukomesha "machafuko kwa utumiaji silaha", mwaka mmoja kukishuhudiwa nchini humo visa vya watu kuuawa kwa kwa kupigwa risasi.

Kutokana na 'wimbi' hili la mauaji, rais Joe Biden kwa mara nyingine tena ameomba jibu kali ili kukomesha 'janga hili la vurugu za bunduki'.
Kutokana na 'wimbi' hili la mauaji, rais Joe Biden kwa mara nyingine tena ameomba jibu kali ili kukomesha 'janga hili la vurugu za bunduki'. © TASOS KATOPODIS / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani alitoa wito siku ya Jumanne kukomesha "mlipuko wa vurugu za bunduki" baada ya "wimbi" la mauaji, na mwaka mmoja baada ya visa vya watu kupigwa, hususa kisa cha watu kadhaa walioawa kwa kupigwa risasi kilichotokea wakati wa gwaride mwaka jana.

Mwaka jana, mwanamume alifyatua risasi wakati wa gwaride lililoandaliwa karibu na Chicago, Illinois wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya kitaifa ya Julai 4, na kuua watu saba na kujeruhi kadhaa, na kubadilisha "siku hii ya fahari ya uzalendo" katika "msiba", amekumbusha Joe Biden.

Jumatatu jioni, mtu mwenye bnduki aliwafyatulia risasi watu kadhaa katika mitaa ya Philadelphia (kaskazini mashariki mwa Marekani) na kuua watu watano, wenye umri wa miaka 15 hadi 59 kulingana na polisi, ambayo ilitangaza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na idara za usalama.

Mshambuliaji huyo alikuwa amejihami kwa bunduki aina ya AR-15 na kuwapiga risasi watu hao "kiholela", kulingana na Kamishna wa Polisi wa Philadelphia Danielle Outlaw.

'Wimbi' la mauaji

Kusini mwa nchi hiyo, huko Texas, watu watatu pia waliuawa kwa silaha za moto na watu wanane kujeruhiwa Jumatatu jioni huko Forth Worth, wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika mkesha wa sherehe za uhuru, kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo. Siku chache kabla, watu wawili waliuawa na wengine 28 kujeruhiwa kwa risasi wakati wa tafrija katika mtaa moja huko Baltimore, pwani ya mashariki ya Marekani.

Akikabiliwa na "wimbi" hili la mauaji, rais Joe Biden kwa mara nyingine tena ameomba jibu kali ili kukomesha "janga hili la vurugu za bunduki".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.