Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Saba wauawa katika mashambulio mawili ya risasi California

Watu saba wameuawa katika matukio mawili ya kupigwa risasi Jumatatu katika shamba la uyoga na katika kampuni ya lori katika jamii ya pwani kusini mwa San Francisco, vyanzo rasmi vimesema.

Maafisa wa polisi wanafungua mlango wa gari nje ya eneo la Torrance, California, ambapo mshukiwa wa mauaji ya watu 10 katika Monterey Park, California, anaaminika amejificha Januari 22, 2023.
Maafisa wa polisi wanafungua mlango wa gari nje ya eneo la Torrance, California, ambapo mshukiwa wa mauaji ya watu 10 katika Monterey Park, California, anaaminika amejificha Januari 22, 2023. AFP - ROBYN BECK
Matangazo ya kibiashara

Mshukiwa mwenye umri wa miaka 67, Zhao Chunli, amekamatwa. Alikuwa "mfanyakazi mwenye hasira," kulingana na mwenyekiti wa Bodi ya Wasimamizi wa Kaunti ya San Mateo Dave Pine.

Amesema watu wanne wameuawa katika shamba hilo na wengine watatu katika kampuni ya lori nje kidogo ya Half Moon Bay, mji ulio umbali wa maili 30 kusini mwa San Francisco, katika jimbo la California.

"Hakuna tishio linaloendelea kwa jamii kwa wakati huu," ofisi ya mkuu wa kaunti hyo imesema.

Matukio hayo yanafuatia vifo vya watu 11 siku ya Jumamosi kwenye ukumbi wa densi katika jimbo hilo la California.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.