Pata taarifa kuu

Mexico: Maiti zaidi ya ishirini zagunduliwa karibu na mpaka wa kaskazini

Shirika linalohusika na kutafuta watu waliotoweka limegundua miili 22 katika makaburi zaidi ya kumi na mbili karibu na mpaka na Marekani.

Kundi linalohusika na kutafuta watu waliotoweka limegundua takriban miili 22 katika makaburi ya siri yaliyoko Reynosa.
Kundi linalohusika na kutafuta watu waliotoweka limegundua takriban miili 22 katika makaburi ya siri yaliyoko Reynosa. DR
Matangazo ya kibiashara

Kundi linalohusika na kutafuta watu waliotoweka limegundua takriban miili 22 katika makaburi ya siri yaliyoko Reynosa Kaskazini Mashariki mwa Mexico, karibu na mpaka na Marekani. Mamlaka imetoa habari hii hivi punde.

"Walipata makaburi kadhaa, 12 kwa jumla, na miili 22," amesema Jorge Cuellar, msemaji wa idara ya usalama katika jimbo la Tamaulipas, ambako Reynosa inapatikana. Ugunduzi huo ulifanywa na kuripotiwa na kundi la Upendo kwa waliotoweka kutoka Tamaulipas, eneo linalopatikana kwenye mpaka na Marekani lililoathiriwa na ghasia zinazohusishwa na uhalifu wa kupangwa. Bw Cuellar ameongeza kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa eneo hilo ndiyo inayosimamia uchunguzi huo na kwamba idadi ya mwisho ya miili itatangazwa baadaye.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa wahanga waliuawa katika makabiliano katika ya vita dhidi ya dawa za kulevya.

Mifupa mingi iliyopatikana ilibaki chini ya ardhi kwa muda wa miezi 10 na 14, amesema. Baada ya kukata tamaa na ukosefu wa matokeo ya uchunguzi, familia za waliotoweka wakati mwingine hujihusisha na kutafuta wapendwa wao, mara nyingi katika maeneo yasiyofaa. Jimbo la Tamaulipas ni eneo linalokumbwa na mapigano ya kudumu kati ya makundi ya wahalifu yanayopigania kutumia barabara kwa usafirishaji wa madawa ya kulevya.

Mnamo mwezi Machi, Wamarekani wanne waliochukuliwa kuwa ni wafanyabiashara wa madawa ya kulevya walitekwa nyara huko Matamoros. Jimbo la Matamoros linashika nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya watu (13,000) waliokosekana katika nchi nzima ya Mexico, nyuma ya Jalisco, ambayo ina watu 14,987 wanaotafutwa mpaka sasa baada ya kuripotiwa kutoweka. Nchi hiyo ina watu 110,000 waliotoweka tangu 1962, tatizo sugu linaloelezwa na Umoja wa Mataifa kuwa janga la kibinadamu".

Pia, matukio 350,000  ya mauaji yamerekodiwa nchini Mexico tangu kuzinduliwa kwa vita vya kijeshi dhidi ya madawa ya kulevya mnamo mwezi Desemba 2006, mengi yakihusishwa na makundi ya wahalifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.