Pata taarifa kuu

Urusi yachukua nafasi ya urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Urusi imechukua wadhifa wa urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi kwa mwezi mzima wa Aprili. Kwa baadhi, urais huu ni kama "fedheha mbele ya jumuiya ya kimataifa" kwa Ukraine na "Siku ya Wajinga" kwa nchi za Magharibi.

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Februari 23, 2023 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Februari 23, 2023 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. © Bebeto Matthews / AP
Matangazo ya kibiashara

"Urusi kuongoza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi wa Aprili ni fedheha mbele ya jumuiya ya kimataifa," Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kouleba amesema kwenye Twitter.

Kulingana na Waziri huyo, "wanachama wa sasa" wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lazima "wazuie jaribio lolote" la Urusi "kutumia vibaya urais wake".

Siku ya Alhamisi, Bw Kouleba aliuita urais huu wa Urusi "mzaha mbaya", akisema kwamba "Urusi imenyakua kiti chake; inaendesha vita vya kikoloni; rais wake ni mhalifu wa vita anayetafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa kuwateka nyara watoto".

Ukosoaji huu kutoka Kiev, hata hivyo, haukuzuia Moscow kuhakikisha kuwa ujumbe wake kwa Umoja wa Mataifa mwezi huu, ambayo imerithi kutoka Msumbiji, utaongozwa na mkuu wa diplomasia ya Urusi, Sergei Lavrov.

"Tukio lingine muhimu la urais wa Urusi litakuwa mjadala wa wazi wa ngazi ya juu wa Baraza la (Usalama) kuhusu "Ufanisi wa pande nyingi kupitia utetezi wa kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa." Mkutano huu utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov," msemaji Maria Zakharova aliwaambia waandishi wa habarisiku ya Alhamisi.

Alibaini kwamba Bw. Lavrov pia ananuia kuongoza kikao cha mijadala kuhusu Mashariki ya Kati mnamo Aprili 25.

- 'Aibu' -

Wafuasi wa kidiplomasia wa Kyiv, hasa Marekani, waliibuka haraka dhidi ya msimamo kama huo.

"Tunatarajia Urusi itaendelea kutumia makao yake makuu kueneza habari potofu na kujaribu kuvuruga kutoka kwa majaribio yake ya kuhalalisha vitendo vyake nchini Ukraine na uhalifu wa kivita ambao wanajeshi wake wanafanya", alisema siku ya Alhamisi msemaji wa Ikulu ya White House, Karine Jean-Pierre.

"Nchi ambayo inakiuka wazi Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuvamia jirani yake haina nafasi katika Baraza la Usalama," ameongeza.

Nchi za Baltic, wafuasi wengine muhimu wa Kyiv na ambao zinapinga vikali Moscow, kwa upande wao wamesema Jumamosi ya "Siku ya Wajinga".

"Siku ya Wajinga ni siku kamili" kwa Urusi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Lithuania imesema. "Urusi, ambayo inaendesha vita vya kikatili dhidi ya Ukraine, inaweza tu kuongoza +Baraza la Usalama+".

Katika Umoja wa Mataifa, Urusi inasema kwa upande wake kukabiliana na "muungano a nchi za magharibi", ambao umeipiga marufuku kutoka mataifa ya dunia tangu kuanza kwa mashambulizi yake ya kijeshi nchini Ukraine Februari 2022.

Mkutano wa kwanza wa Baraza la Usalama chini ya urais wa sasa wa Urusi utafanyika Jumatatu asubuhi, lakini itakuwa tu mijadala ya faragha ya mpango wa kazi wa mwezi huo.

Itafuatwa, kama kawaida, na mkutano wa waandishi wa habari na rais mpya wa baraza hili, balozi wa Urusi Vassili Nebenzia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.