Pata taarifa kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lalani Urusi kunyakuwa majimbo manne ya Ukraine

Umoja wa Mataifa umepiga kura kulaani hatua ya Urusi kuandaa kura ya maoni na kuchukua majimbo manne ya Ukraine kinyume na sheria za Kimataifa, na kutaka dunia kutotambua hatua hiyo. 

Kura kuhusu "unyakuzi haramu" wa Urusi nchini Ukraine katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Oktoba 12, 2022.
Kura kuhusu "unyakuzi haramu" wa Urusi nchini Ukraine katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Oktoba 12, 2022. © Bebeto Matthews/AP
Matangazo ya kibiashara

Kati ya nchi wanachama 193, nchi 143 zimepiga kura kulaani hatua hiyo na kusisitiza kuwa inaitambua Ukraine kama nchi huru na kutambua mipaka yake ya Kimataifa. 

Awali Urusi ilishindwa katika juhudi zake za kutaka kura hii ipigwe kwa siri. Kabla ya kura hiyo kupigwa, Marekani ilifanya juhudi kubwa za kidiplomasia kuzishawishi Afrika Kusini na India ziunge mkono azimio hilo lakini haikufanikiwa.

Hii ndio kura katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambayo imeungwa mkono na nchi nyingi zaidi, kati ya nne ambazo tayari zimefanyika katika baraza hilo tangu Urusi kuivamia Ukraine mwezi Februari.

Wakati hayo yakijiri, Jumuiya ya kijeshi ya nchi za Maghairbi NATO imesema imeipa Ukraine mitambo ya kuzuia mashambulio ya angaa, baada ya Urusi kuendeleza mashambulio yake katika miji mbalimbali za nchi hiyo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.