Pata taarifa kuu

Viongozi wa G7 kuendelea kushikamana na kusaidia Ukraine

Viongozi kutoka mataifa tajiri duniani, ya G7 wameapa kuendelea kuiunga Ukraine  kwa kipindi kirefu kijacho ili kuendelea kupambana na Urusi ambayo imeendelea kuishambulia. 

Viongozi wa G7 wakisikiliza maoni ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye alizungumza kwa njia ya video, Juni 27, 2022.
Viongozi wa G7 wakisikiliza maoni ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye alizungumza kwa njia ya video, Juni 27, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Msimamo huu wa pamoja umekuja baada ya viongozi wa nchi hizo kukutana kwa njia ya vídeo hap jana, wamesema wtaendelea kuisaidia na silaha za vita na misaada nyingine ya kibinadamu. 

Mbali na viongozi hao wa G 7, jeshi la kujihami la Mataifa ya Magharibi NATO nalo limeasema litaendelea kusimama na Ukraine katika kipindi chote cha vita. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliyehotubia vingozi hao, alienda kuomba msaada zaidu wa silaha za kijeshi, huku akisema hakuna uwezekano wa kuzungumza na kiongozi wa Urusi. 

Mkutano huu umefanyika baada ya watu 19 kuuawa na wengine kujeruhiwa baada ya makombora ya Urusi, kushambulia miji mbalimbali ya Ukraine likiwemo jiji kuu Kiev. 

Katika hatua nyingine, kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko, mshirika wa karibu wa rais Vladimir Putin amekubali kutuma jeshi lake katika mpaka na Ukraine, kwa kile alichosema ni kujilinda dhidi ya hatari inayoweza kutoka jijiji Kiev. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.