Pata taarifa kuu

Kyiv yakumbwa na mashambulizi, Urusi yaonya mataifa ya magharibi

Urusi imeendelea kulaaniwa kwa kushambulia miji kadhaa ya Ukraine, likiwemo jiji kuu Kyiv kwa mara ya kuanza.

Katikati mwa jiji la Kyiv baada ya mashambulizi ya anga ya Urusi, Oktoba 10, 2022.
Katikati mwa jiji la Kyiv baada ya mashambulizi ya anga ya Urusi, Oktoba 10, 2022. © REUTERS / VALENTYN OGIRENKO
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Joe Biden amesema nchi yake itaendelea kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi na kulinda watu wake, baada ya  mashambulio ya jijini Kiev, kulenga chuo kikuu na uwanja wa watoto kuchezea. 

Rais Joe Biden wa Marekani ameahidi kuipa Ukraine mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga, muda mfupi baada ya Ukraine kusema inahitaji kuimarisha zaidi mifumo yake ya anga. Washington imesema mifumo hiyo itaanza kuwasilishwa kuanzia miezi miwili ijayo ama zaidi.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa watu wengi huenda wakakimbia nchini Ukraine kwa sababu ya mashambulio hayo. 

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema mashambulio hayo ni kulipiza kisiasa baada ya kushambuliwa kwa daraja katika eneo la Crimea Jumamosi iliyopita. 

Wakati huo huo Urusi imesema itakabiliana na hatua ya mataifa ya Magharibi yanayoongea ushiriki wao katika vita vya Ukraine, hata kama haitaki kupambana moja kwa moja na Muungano wa Kijeshi wa NATO. Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Ryabkov, baada ya Washington kuahidi misaada zaidi wa kijeshi kwa Kyiv.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.