Pata taarifa kuu

Mashambulizi ya Urusi Ukraine: Umoja wa Mataifa walaani "ongezeko lisilokubalika la vita"

Miji mingi imeshambuliwa kwa mabomu nchini Ukraine Jumatatu asubuhi Oktoba 10, mji mkuu wa Kyiv ukilengwa na mashambulizi ya anga ya kwanza kwa zaidi ya miezi mitatu. Takriban watu 10 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa. 

Gari limeteketea kwa moto baada ya shambulio la Urusi huko Kyiv, Ukraine, Jumatatu, Oktoba 10, 2022.
Gari limeteketea kwa moto baada ya shambulio la Urusi huko Kyiv, Ukraine, Jumatatu, Oktoba 10, 2022. AP - Roman Hrytsyna
Matangazo ya kibiashara

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema "ameshangazwa sana" na mashambulizi haya, msemaji wake amesema katika taarifa. Mashambulizi haya ni "ongezeko jipya lisilokubalika la vita" ambalo raia "hulipa bei kubwa zaidi".

Miji ya Khmelnytskyï, Lviv, Dnipro, Vinnitsia, Zaporijgia, Soumi, Kharkiv au hata Zhytomyr imekumbwa na mashambulizi ya anga kama inavyothibitishwa na watumiaji wengi wa Intaneti wanaochapisha picha na video za kuvutia za Jumatatu hii, Oktoba 10.

Akiwa amekabiliwa na mashambulizi ya Urusi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anaomba mkutano wa dharura wa G7 ufanyike Jumanne hii, Oktoba 11. Hayo yanajiri wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin anaahidi majibu "makali" katika tukio la mashambulizi mapya ya Ukraine dhidi ya Urusi.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameshutumu "ongezeko lisilokubalika la vita" nchini Ukraine.

Video nyingi za milipuko hiyo zimeendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Miji ya Khmelnytskyï, Lviv, Dnipro, Vinnitsia, Zaporijgia, Soumi, Kharkiv au hata Zhytomyr imekumbwa na mashambulizi hayo ya anga kama inavyothibitishwa na watumiaji wengi wa Intaneti wanaochapisha picha na video za kuvutia za Jumatatu hii, Oktoba 10.

Kwa upande wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa ziara yake huko Château-Gontier (Mayenne), amesema kwamba atawaleta pamoja washauri wake wa kidiplomasia na kijeshi mara tu atakaporejea Paris "kuchunguza" hali ya Ukraine na akataja "mabadiliko makubwa" katika asili" ya vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.