Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Daraja la Crimea ladondoka baada ya mlipuko mkali

Bomu lililotegwa ndani ya gari liliwasha moto mkubwa kwenye Daraja la Crimea, miundombinu muhimu na ishara ya kunyakuliwa kwa rasi ya Ukraine, Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Ugaidi ya Urusi imetangaza Jumamosi, bila kuishutumu Ukraine mara moja. Inasadikiwa kuwa angalau watatu wamefariki kulingana na Moscow.

Sehemu ya Daraja la Crimea likiwaka moto. Tarehe 8 Oktoba 2022.
Sehemu ya Daraja la Crimea likiwaka moto. Tarehe 8 Oktoba 2022. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

“Kwa mujibu wa takwimu za awali, watu watatu wameuawa kutokana na ajali hiyo. Pengine ni abiria wa gari lililokuwa karibu na lori lilipolipuka,” Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imesema kwenye taarifa.

Picha zinazosambaa mtandaoni kutoka kwenye daraja zinaonyesha njia ya reli ikiwaka moto kwa makumi ya mita na sehemu ya barabara meporomoka. Daraja hili, lililojengwa kwa gharama kubwa kwa agizo la Vladimir Putin kuunganisha rasi iliyounganishwa na Urusi, linatumiwa hasa kusafirisha vifaa vya kijeshi kutoka kwa jeshi la Urusi linalopigana nchini Ukraine.

Ikiwa Ukraine inahusika na mkasa huo na mlipuko kwenye Daraja la Crimea, ukweli kwamba miundombinu muhimu kama hiyo kutoka mbele inaweza kuharibiwa na vikosi vya Ukraine itakuwa chuki kwa Moscow. Hasa tangu Urusi imekuwa ikishindwa kufanya vizuri kijeshi tangu mwanzoni mwa mwezi Septemba, wanajeshi wake wakilazimika kurudi nyuma kaskazini mashariki na kusini mwa nchi hiyo, hasa katika jimbo la Kherson, linalopakana na Crimea, ambalo Vladimir Putin amedai kuliunganisha na nchi yake.

"Leo saa 06:07 (03:07 UT) kwenye barabara sehemu ya Daraja la Crimea (...) bomu lililotegwa kwenye gari lililipuka na kusababisha matangi saba ya reli yaliyokuwa yakienda Crimea kuteketea kwa moto," kamati hiyo imesema, ikinukuu mashirika ya habari ya Urusi. Msemaji wa Kremlin ameliambia shirika la habari la Ria Novosti kwamba Vladimir Putin ameagiza kuundwa kwa tume ya serikali ili kubaini ukweli. Kulingana na Kamati ya Kupambana na Ugaidi, njia mbili za barabara zimeharibika, lakini upinde wa daraja haukuathiriwa. Usafiri wa treni na magari umesitiishwa, na feri zimeanza kufanya kazi ili kuwezesha watu, mali na vitu kuvuka, kulingana na mashirika ya habari ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.