Pata taarifa kuu

Vitisho vya Urusi: Joe Biden aonya juu ya hatari ya 'maangamizi ya nyuklia'

Wakati Urusi ikitishia kutumia silaha zake za nyuklia katika vita vya Ukraine, Rais wa Marekani Joe Biden alisema siku ya Alhamisi, Oktoba 6, kwamba "sio masihara" na amekumbusha kwamba kitisho cha rais wa Urusi Vladimir Putin kutumia zana za nyuklia, ndicho kitisho kikubwa zaidi cha aina hiyo tangu mzozo wa makombora ya Cuba.

Kwa mara ya kwanza tangu Vita Baridi, Rais wa Marekani Joe Biden ameonya juu ya hatari ya "maangamizi ya nyuklia", Alhamisi, Oktoba 6, 2022.
Kwa mara ya kwanza tangu Vita Baridi, Rais wa Marekani Joe Biden ameonya juu ya hatari ya "maangamizi ya nyuklia", Alhamisi, Oktoba 6, 2022. REUTERS - TOM BRENNER
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Joe Biden amesema Vladimir Putin hakuwa akifanya masihara alipozungumzia "uwezekano wa matumizi ya silaha za nyuklia za kimbinu au silaha za kibayolojia au za kemikali", kwa sababu jeshi lake "halifanyi kazi vizuri". Na rais wa Marekani kuibua "hatari ya kutumia silaha za nyuklia kwa mara ya kwanza tangu mgogoro wa makombora ya Cuba, ikiwa mambo yataendelea kufuata njia inayotumiwa kwa sasa".

Ilikuwa katika kurejelea mzozo huu wa mwaka 1962 na hatari ambayo rais wa Marekani ametumia usemi wa "maangamizi ya nyuklia" ("Nuclear Armageddon").

"Ni mlango gani wa kutokea kwa Putin"

Gazeti la New York Times linasema kwamba, kwa miaka sitini, marais wa Marekani wamezungumza mara chache na kwa sauti ya chini juu ya uwezekano wa matumizi ya silaha za nyuklia. Joe Biden amesema hayo katika zoezi la uchangishaji fedha kwa wagombea wa Bunge la Seneti kutoka chama cha Democratic. 

Joe Biden aliwaambia wafadhili wa chama cha Democratic mjini New York kwamba kwa mara ya kwanza tangu mgogoro wa makombora ya Cuba, ulimwengu unakabiliwa na kitisho cha moja kwa moja cha matumizi ya silaha za nyuklia. 

Mwishoni mwa mwezi wa Septemba, mshauri wake wa usalama alikuwa tayari amesisitiza kwamba matumizi yoyote ya silaha za nyuklia yatakuwa na madhara makubwa kwa Urusi. "Tunajaribu kuelewa ni mlango gani wa kutokea kwa Putin," alieleza rais wa Marekani siku ya Alhamisi. "Anawezaje kuondoka katika hali hii, ajipange vizuri ili asipoteze utawala wake nchini Urusi? "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.