Pata taarifa kuu

Urusi yatambua rasmi majimbo manne ya Ukraine kama maeneo yake

Rais Vladimir Putin, ametia saini sheria inayotambua majimbo manne ya Ukraine ya Donetsk, Lugansk, Kherson na  Zaporizhzhia, kuwa sehemu ya Urusi, licha ya hatua hiyo kushtumiwa na mataifa ya Magharibi, ikiwemo Umoja wa Mataifa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow, Februari 19, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow, Februari 19, 2022. © via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Mbali na hatua hiyo, rais Putin, ametia saini agizo la kuwateua viongozi kutoka Urusi wanaoongoza majimbo hayo , kukaimu uongozi wa maeneo hayo, na kueleza kuwa anatumaini, yatapata utulivu. 

Hatua hii imekuja, baada ya mabunge yote mawili, kujadili na kuunga mkono uamuzi wa Urusi kuchukua majimbo hayo ya Ukraine. 

Mwishoni mwa mwezi uliopita, wakaazi wa majimbo hayo waliandaa kura hiyo ya maoni iliyoandaliwa na Urusi ili kuamua upande wa nchi hiyo, kitendo ambacho Ukraine inasema raia wake walilazimishwa. 

Wakati hayo yakijiri, kiongozi wa Urusi katika jimbo la Kherson amesema wanajeshi wa nchi yake wanajipanga upya baada ya vikosi vya Ukraine kuchukua maeneo kadhaa, wakati huu Kiev ikisema wanajeshi wake wanaelekea katika maeneo kadhaa ya Luhansk, yanayodhibitiwa na wanajeshi wa Urusi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.