Pata taarifa kuu

Rais wa Ukraine akataa katu katu kufanya mazungumzo na mwenzake wa Urusi

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ametia saini azimio, linalosema kutowepo kwa mpango wa kufanya  mazungumzo na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa rais Zelenskyy, unakuja baada ya tarifa kuwa, Urusi ilikuwa imewaandaa wanajeshi zaidi ya Laki mbili wa akiba, kwenda kuendelea na mapigano nchini Ukraine. 

Wakati hayo yakiri, bunge la Urusi limepitisha azimio la kutambua majimbo manne ya Ukraine, kuwa sehemu ya Urusi. 

Licha ya hatua hii kulaaniwa na Ukraine na Mataifa ya Magharibi ukiwemo Umoja wa Mataifa, rais Putin anatarajiwa kumalizia mchakato wa kuyaingiza majimbo ya Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhia kuwa sehemu ya Urusi. 

Umoja wa Ulaya, umemwita Balozi wa Urusi katika Jumuiya hiyo, kusisitiza pingamizi la Urusi kuchukua majimbo hayo manne baada ya kufanyika kwa kura ya maoni wiki iliyopita, zoezi inalosema ni kiyume cha sheria za Kimataifa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.