Pata taarifa kuu

Wanaharakati wa haki za binadamu watunukiwa Tuzo ya amani ya Nobel

Kamati ya Nobel imeamua kutoa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2022 kwa mtetezi wa haki za binadamu wa Belarus Ales Bialiatski, lakini pia kwa shirika lisilo la kiserikali la Memorial na shirika la haki za binadamu la Ukraine Center for Civil Liberties. Washindi watatu ambao, kulingana na kamati ya Nobel, "wanafufua na kuheshimu maono ya Alfred Nobel ya amani na udugu kati ya mataifa, maono ambayo ulimwengu unahitaji zaidi leo".

Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2022 imetunukiwa kwa pamoja mwanaharakati wa haki za binadamu wa Belarus Ales Bialiatski, Shirika lisilo la kiserikali lisilo la Haki za Binadamu la Urusi Memorial na shirika la Haki za Binadamu nchini Ukraine la Center for Civil Liberties.
Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2022 imetunukiwa kwa pamoja mwanaharakati wa haki za binadamu wa Belarus Ales Bialiatski, Shirika lisilo la kiserikali lisilo la Haki za Binadamu la Urusi Memorial na shirika la Haki za Binadamu nchini Ukraine la Center for Civil Liberties. © The Nobel Prize
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Nobel ilichagua kutunukia "watetezi watatu bora wa haki za binadamu, demokrasia na kuishi pamoja kwa amani katika nchi tatu jirani za Belarus, Ukraine na Urusi".

Ales Bialiatski ni mwanaharakati wa kisiasa anayejulikana kwa kazi yake kama mkuu wa Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Viasna, shirika kuu la haki za binadamu nchini Belarus. Kwa sasa yuko kizuizini na amezuiliwa mara kadhaa kwa shughuli zake kama mtetezi wa haki za binadamu. Mkewe amesema "ameshindwa kujizuia na hisia" na kutoa"shukrani", wakati kiongozi wa upinzani Svetlana Tikhanovskaya akibaini kwamba "tuzo ni utambuzi muhimu kwa Wabelarus wote wanaopigania uhuru na demokrasia".

Sisi wafungwa wa kisiasa tuko chini ya utawala mkali zaidi. Haki zetu zinakiukwa bila sababu. Kwa mfano, nilinyimwa uwezekano wa kupokea vifurushi au kutembelewa na mke wangu..., amesema Ales Bialiatski mwaka 2014 akihojiwa na Véronique Gaymard.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.