Pata taarifa kuu

Unyakuzi wa Urusi dhidi ya Ukraine: Waziri wa mambo ya nje wa Madagascar afutwa kazi

Richard Randriamandranto amefutwa kazi na Rais wa Madagascar. Waziri wa Mambo ya Nje anashutumiwa kwa kuchukua, peke yake, uamuzi wa kupiga kura kuunga mkono azimio la kulaani "unyakuzi haramu wa Urusi dhidi ya majimbo maanne ya Ukraine", Madagascar ambayo hadi sasa imekuwa ikionyesha msimamo wa kutoegemea upande wowote katika kura za awali. 

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York mnamo Oktoba 12, 2022.
Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York mnamo Oktoba 12, 2022. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Alipohojiwa na RFI, ambaye Richard Randriamandranto amethibitisha habari hiyo na kuongeza "baada ya kufanya uamuzi huu: “sidhani kuwa nilihatarisha maslahi ya taifa kwa kupiga kura hiyo. Historia itawahukumu wengine,” alimalizia.

Kwa umuazi huo, Madagascar iliungana na nchi zingine 142 kwa kulaani unyakuzi huo wa Urusi wakati wa kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, mtandaoni. 

Lengo rasmi la kulaaniwa kwa Urusi kwa uamuzi wake ni " kura za maoni haramu zilizofanywa katika majimbo manne ya Ukraine na unyakuzi haramu wa majimbo hayo manne, uamuzi uliofanywa na Urusi". Chaguo ambalo liliiweka Madagascar upande wa nchi za magharibi dhidi ya vita hivi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.