Pata taarifa kuu

UNICEF: Vita nchini Ukraine na mfumuko wa bei vinawaingiza mamilioni ya watoto katika umaskini

Kulingana na utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) uliochapishwa Jumatatu tarehe 17 Oktoba, vita vya Ukraine na kupanda kwa gharama ya maisha kumesababisha mamilioni ya watoto zaidi kukabiliwa na umaskini katika Ulaya Mashariki na Asia ya Kati katika miezi ya hivi karibuni.

Watoto wanatazama nje kupitia dirisha la treni mjini Kyiv, Ukraine, Machi 3, 2022.
Watoto wanatazama nje kupitia dirisha la treni mjini Kyiv, Ukraine, Machi 3, 2022. Associated Press - Vadim Ghirda
Matangazo ya kibiashara

Katika Ulaya Mashariki na Asia ya Kati, "vita nchini Ukraine na kupanda kwa mfumuko wa bei vimewasukuma watoto milioni nne zaidi kukumbwa na umaskini, ongezeko la 19% tangu 2021", unasema utafiti wa UNICEF, ambao unabaini kwamba watoto wanakabiliwa na na hali ngumu ya maisha kutokana na mdororo wa kiuchumi unaosababishwa na mzozo huo. Ingawa wanawakilisha 25% ya raia, wanachukua karibu 40% ya watu milioni 10.6 wa ziada wanaoishi katika umaskini mwaka huu, unabainisha utafiti huu unaojumuisha nchi 22.

Urusi, moja ya nchi zilizoathirika zaidi

Ukweli unaojulikana, Urusi, ikiwa na watoto milioni 2.8 wa ziada wanaoingia kwenye umaskini, inachangia karibu robo tatu ya jumla ya ongezeko lililorekodiwa na UNICEF. Sababu mbili zinaelezea hali hii: Urusi ina idadi kubwa ya watu na UNICEF ​​​​inakadiria kuwa Pato la Taifa la nchi litashuka kwa 8%, kushuka kwa pili kwa ukubwa kati ya nchi zilizojumuishwa katika uchambuzi. "Athari za mzozo wa Ukraine ni muhimu sana nchini Urusi, kwa sababu vita vinasababisha ufikiaji duni wa idadi fulani ya bidhaa za kimsingi, mafuta au kusahihisha tu uwezo wa ununuzi kutokana na mfumuko wa bei," ameliambia shirika la habari la AFP Adeline Hazan, mkuu wa UNICEF nchini ​​Ufaransa.

Kwa upande wake, Ukraine ina watoto nusu milioni wa ziada wanaoishi katika umaskini, ambayo inashika nafasi ya pili, ikifuatiwa na Romania yenye watoto 110,000 wa ziada, utafiti unabainisha. "UNICEF inatahadharisha kuhusu athari ya vita hivi na kutoa wito kwa serikali kutoa msaada wa nguvu juu ya ulinzi wa kijamii na kutekeleza programu za usaidizi wa pesa taslimu kwa familia zilizo hatarini zaidi zenye watoto." Anaongeza Bi. Hazan.

Matatizo ya ziada kwa watoto maskini zaidi

Kwa sababu athari za umaskini kwa watoto zinaenda mbali zaidi ya mfumo pekee wa matatizo ya kifedha ya familia: kadiri familia inavyozidi kuwa maskini, ndivyo sehemu kubwa ya mapato yake yanavyotolewa kwa mahitaji ya msingi kama vile chakula na mafuta. Na wakati gharama ya bidhaa za kimsingi inapopanda, pesa zinazopatikana kwa mahitaji mengine kama vile afya na elimu hupungua. Matokeo yake, watoto maskini zaidi wana nafasi ndogo ya kupata huduma muhimu na wako katika hatari zaidi ya ukatili na unyanyasaji, linaeleza shirika la Umoja wa Mataifa.

Kuongezeka kwa umaskini wa watoto katika Ulaya Mashariki na Asia ya Kati kunaweza kusababisha vifo vya watoto 4,500 zaidi kabla ya siku yao ya kuzaliwa kwa mara ya kwanza na kusababisha upungufu wa elimu kwa watoto 117,000 zaidi walioacha shule mwaka 2022 pekee, inaonya UNICEF katika ripoti hii.

(pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.