Pata taarifa kuu

UN yainyooshea kidole cha lawama Urusi kwa kuhamisha watoto kutoka Ukraine

Kuna 'mashtaka ya kuaminika' ya watoto waliohamishwa kwa nguvu kutoka Ukraine kwenda Urusi, amesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, akielezea wasiwasi wake juu ya uwezekano wao wa kuasili na familia za Warusi.

Watoto wanawasili kwa gari katika kituo cha mpaka cha Medyka nchini Poland Jumatano, Machi 2, 2022, baada ya kutoroka Ukraine.
Watoto wanawasili kwa gari katika kituo cha mpaka cha Medyka nchini Poland Jumatano, Machi 2, 2022, baada ya kutoroka Ukraine. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

"Kuna shutuma za kuaminika za kuhamishwa kwa nguvu kwa watoto waliotenganishwa na wazazi wao na kwenda katika eneo linalokaliwa na Urusi au kwa Shirikisho la Urusi lenyewe," Ilze Brands Kehris ameuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

"Tuna wasiwasi kwamba mamlaka ya Urusi imepitisha utaratibu uliorahisishwa wa kutoa uraia wa Urusi kwa watoto ambao hawako chini ya uangalizi wa wazazi wao, na kwamba watoto hawa wanastahili kuasiliwa na familia za Kirusi," ameongeza.

Marekani yamfungulia mashtaka Vladimir Putin

Marekani, mwanzoni mwa mkutano huu wa Baraza la Usalama na Albania, ilishutumu moja kwa moja ofisi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatano kwa kuandaa moja kwa moja uhamishaji wa kulazimishwa wa maelfu ya Waukraine kwenda Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.