Pata taarifa kuu

Ushindi wa Lula nchini Brazili: Norway yatangaza kuanza tena ushirikiano wake

Norway, ambayo ilikuwa imezuia msaada wake wa kifedha dhidi ya ukataji miti wa Amazon nchini Brazili chini ya utawala wa rais Jair Bolsonaro, itaanza tena ushirikiano wake na Brasilia baada ya ushindi wa Lula, Waziri wa Mazingira wa Norway amesema Jumatatu (Oktoba 31).

Luiz Inaciao Lula da Silva, rais teule wa Brazil, hapa kwenye picha alikuwa Paris, Novemba 16, 202.
Luiz Inaciao Lula da Silva, rais teule wa Brazil, hapa kwenye picha alikuwa Paris, Novemba 16, 202. © AFP - JULIEN DE ROSA
Matangazo ya kibiashara

"Tulikuwa na ushirikiano mzuri na wa karibu sana na serikali kabla ya Bolsonaro na ukataji miti nchini Brazil ulipunguwa kwa kasi katika utawala wa Lula da Silva", amebaini Espen Barth Eide. "Kisha tukaingia kwenye mzozo wa mbele na Bolsonaro ambaye alikuwa na chaguo linalopingana kabisa na suala la kutokata miti".

"Kashfa"

Mfadhili mkuu wa ulinzi wa msitu wa Amazoni, nchi ya Scandinavia, kama Ujerumani - nchi nyingine inayotoa msaada mwingine mkubwa wa kifedha - - ilisimamisha msaada wake kwa Brazil mnamo 2019, mwaka ambao Jair Bolsonaro alichukua hatamu ya uongozi wa nchi. Chini ya utawala wa itikadi kali za mrengo wa kulia, ukataji miti wa msitu wa Amazon umeongezeka kwa 70%, takwimu "mbaya" amesema Bw. Barth Eide.

Kulingana na waziri huyo, pesa za Norway bilioni 5 (sawa na euro milioni 487) za msaada wa Norwayambazo zinatarajiwa leo, hazijatumika, kwenye Mfuko wa kuhifadhi msitu wa Amazon. "Kuhusu Lula, tunaona kwamba, wakati wa kampeni, alisisitiza uhifadhi wa msitu wa Amazoni na ulinzi wa wakazi wa kiasili wa Amazonia," amesema waziri wa Norway katika mahojiano ya simu na shirika la habari la AFP.

"Kuanzisha tena ushirikiano"

“Ndiyo maana tunatazamia kuwasiliana na timu zake haraka iwezekanavyo ili kujiandaa kwa ajili ya kurejesha ushirikiano mzuri wa kihistoria kati ya Brazil na Norway,” ameongeza. Luiz Inacio Lula da Silva ambaye alikuwa rais kati ya mwaka 2003 na mwaka 2011, alihakikisha baada ya ushindi wake kwenye kiti cha urais siku ya Jumapili kwamba Brazil "iko tayari kuchukua nafasi za uongozi tena katika vita dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi". "Brazili na dunia zinahitaji Amazon kuwa hai," alisisitiza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.