Pata taarifa kuu

Raia wa Brazil, wapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria

Raia wa Brazil, wamepiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi unaotarajiwa kuwa wa upinzani mkali kati ya rais wa sasa, Jair Bolsonaro na rais wa zamani wa taifa hilo Luiz Inacio Lula da Silva.

Lula da Silva akiwa na mwenzake rais Bolsonaro, hapa ilikuwa kwenye moja ya midahalo ya televisheni.
Lula da Silva akiwa na mwenzake rais Bolsonaro, hapa ilikuwa kwenye moja ya midahalo ya televisheni. AFP - MAURO PIMENTEL
Matangazo ya kibiashara

Ni uchaguzi ambao wadadisi wa masuala ya siasa za kimataifa wanasema ni vigumu kutabiri nani ataibuka mshindi kutokana na matokeo ya duru ya kwanza ambayo hayakutoa mshindi wa jumla.

Wagombea wote wawili walipiga kura asubuhi ya siku ya Jumapili, wote wakieleza kuwa na tumaini la kuibuka mshindi, baada ya kampeni zilizokuwa zimetawalia na ubabe pamoja na matusi kutoka kwa kambi zote.

Kwa mujibu wa baadhi ya raia waliopiga kura mapema, walisema huu umekuwa moja ya uchaguzi ambao haujawahi kushuhudiwa kwenye taifa hilo.

Hata hivyo kama ilivyo kwa raia wengi wa taifa hilo, baadhi wana hofu kuwa huenda ikiwa Bolsonaro atashindwa atakataa kukubali matokeo sawa kwa mpinzani wake.

Licha ya kuwa hakuna uwezekano mkubwa wa kutokea fujo baada ya matokeo ya mwisho, wachambuzi wengi wanaona kuwa huenda kukawa na vurugu za hapa na pale kulingana na mgombea atakayetangazwa mshindi.

Lula ambaye alishinda duru ya kwanza kwa asilimia 52, Bolsonaro alipata asilimia 48 matokeo yaliyoonesha kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa ushindani.

Akihojiwa baada ya kupiga kura kwenye kitongoji cha Rio, rais Bolsonaro aliyesindikizwa na mamia ya wafuasi wake, alisema "naamini nitashinda".

Katika hatua nyingine, mpinzani wake da Silva, aliyepiga kura kwenye mji wa sao Paulo, alieleza kuridhishwa na zoezi lilivyoendeshwa, akisisitiza imani yake ya kuibuka na ushindi.

Masuala makubwa katika uchaguzi huu yalikuwa ni kuhusu demokrasia na ulinzi wa mazingira hasa msitu wa Amazon, ambao rais Bolsonaro anatuhumiwa kuuharibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.