Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Brazil iliyogawanyika yafanya uchaguzi kumchagua rais wake mpya

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa Jumapili hii asubuhi nchini Brazil ambapo wapiga kura milioni 156 wametakiwa kuchagua kati ya Rais anayemaliza muda wake Jair Bolsonaro na Rais wa zamani Lula, mwenye umri wa miaka 77 na ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi huo.

Wabrazili wakisubiri zamu yao ya kupiga kura katika huko Rocinha, mjini Rio de Janeiro, wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais, Jumapili hii, Oktoba 30, 2022.
Wabrazili wakisubiri zamu yao ya kupiga kura katika huko Rocinha, mjini Rio de Janeiro, wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais, Jumapili hii, Oktoba 30, 2022. AP - Bruna Prado
Matangazo ya kibiashara

Hali inaweza kubadilika katika dakika za mwisho kwani waamuzi ni wapiga kura katika uchaguzi huu ambao ulikuwa na upinzani mkali kati ya wagombea hao wawili.

Jumapili hii Oktoba 29 ni siku muhimu kwa uchaguzi wa urais nchini Brazil, baada ya kampeni zenye ushindani mkali kati ya vigogo wawili wanaotofautiana, viongozi wawili maarufu ambao kila mmoja huleta pamoja karibu nusu ya wapiga kura, anaripoti mwandishi wetu maalum, Achim Lippold. Kwa hivyo zoezi la uhesabiji kura linaweza kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

Lula da Silva alipiga kura asubuhi katika kituo cha kupigia kura cha São Bernardo do Campo huko São Paulo, pamoja na maafisa kadhaa wa chama chake. Alisema ana na "imani kwa ushindi wa demokrasia". Iwapo atashinda, atakuwa rais wa kwanza kurejea madarakani baada ya kuwa tayari amehudumu kwa mihula miwili.

Na ikiwa Jair Bolsonaro atashinda kura, mpinzani wake atakuwa rais wa kwanza kupoteza duru ya pili baada ya kushinda ya kwanza.

Rais wa sasa pia amepiga kura, mapema Jumapili hii asubuhi, katika wilaya ya kijeshi ya Rio de Janeiro. Kwa kumbukumbu, jeshi ni mwangalizi rasmi na litaripoti baada ya kupiga kura, kama anavyotukumbusha mwandishi wetu wa Rio de Janeiro, Sarah Cozzolino.

 Sauti za wapiga kura

Ni Brazil iliyogawanyika ambayo inafanya uchaguzi. Wafuasi wa kila mgombea wanasubiri kuona nanai atakaye shinda uchaguzi huu; wanaogopa madhara makubwa ikiwa mpinzani atashinda.

Wanaomuunga mkono Lula wana wasiwasi kuhusu mustakabali wa demokrasia ikiwa mrengo wa kulia utasalia madarakani. Na Wafuasi wa Bolsonaro wanaamini kwamba kwa Chama cha Wafanyakazi kurejea madarakani, nchi yao itakuwa Venezuela mpya.
Miaka minne iliyopita, nilimpigia kura Bolsonaro lakini usimamizi wake kwa janga la Uviko kulinikatisha tamaa. Lakini pia sintapoteza kura yangu kwa kumpigia kura mwizi. Ni aibu kwa nchi yetu.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.