Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais Brazili: Mjadala mkali wa mwisho wafanyika kati ya Lula na Bolsonaro

Siku mbili kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Brazil, Lula na Jair Bolsonaro walikabiliana vikali katika mdahalo wa mwisho wa televisheni Ijumaa hii jioni, katika mfumo wa mgongano wa mahasimu hao wawili.

Lula (kushoto) na Jair Bolsonaro wakati wa mjadala wa kwanza wa urais mnamo Oktoba 16.
Lula (kushoto) na Jair Bolsonaro wakati wa mjadala wa kwanza wa urais mnamo Oktoba 16. REUTERS - MARIANA GREIF
Matangazo ya kibiashara

Wagombea hao wawili waliitana kila mmoja kuwa muongo angalau mara ishirini wakati wa sehemu ya kwanza ya mdahalo huo uliorushwa kwenye televisheni ya TV Globo, televisheni inayotazamwa zaidi nchini. Kipindi hiki kilidumu kwa muda wa saa mbili na nusu za mabadilishano.

Lula, ambaye alikuwa amevalia suti ya bluu, tai nyekundu, wakati mwingine alivaa miwani, hali ambayo ilimpa sura ya profesa, hasa alipozungumzia sera ya kigeni.

"Uliitenga Brazili. Brazil leo imetengwa zaidi kuliko Cuba. Chini ya serikali yako, Brazil imekuwa nini? Brazil imekuwa uchafu"

Jair Bolsonaro alijibu na kumshambulia mpinzani wakekuhusiana na ufisadi na kumshutumu Lula kwa uhusiano na walanguzi wa dawa za kulevya. Zaidi ya yote, aliangazia rekodi yake ya kiuchumi: "Tuko tayari kufanya kinachowezekana ili kuifanya Brazili kuwa taifa kubwa katika suala la uchumi. Tuna Bunge ambalo linatuunga mkono kikamilifu. Kila kitu kiko tayari kwa kuondoka. Ukuaji wetu utakuwa juu zaidi kuliko ule wa China”.

Wakati huo huo mgombea aliyechaguliwa tena hata hivyo alihitimisha mjadala kwa kutoa kauli ya kushangaza. “Asante sana Mungu wangu. Na ikiwa yote hayo ni kwa mapenzi yako, nitakuwa tayari kutekeleza agizo jipya la mbunge wa shirikisho”, kabla ya kukosoa kauli yake na kusema: “Rais wa Jamhuri”.

Jair Bolsonaro alikuwa mbunge kwa miaka 28, kabla ya kushinda uchaguzi wa urais mwaka wa 2018. Hakuna uhakika kwamba utendakazi wake katika mjadala uliopita utamruhusu kushinda muhula mpya wa urais. Lula, 77, amepanda kidogo kwa kuongeza kura (kutoka pointi nne hadi sita) kuongoza katika kura ya maoni ya hivi punde zaidi ya taasisi ya Datafolha, iliyochapishwa Alhamisi, huku ikionyesha kuwa Lula atapata 53% ya kura, dhidi ya 47% ya rais wa mrengo wa kulia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.