Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Brazil: Mjadala wa mwisho kufanyika kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Brazil itafanyika Jumapili, lakini kuanzia Ijumaa hii jioni, vinara wawili Jair Bolsonaro na Lula watachuana katika mdahalo wa mwisho wa televisheni unaotarajiwa.

Rais wa zamani Lula na Rais wa sasa Jair Bolsonaro wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Brazili, Oktoba 16, 2022.
Rais wa zamani Lula na Rais wa sasa Jair Bolsonaro wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Brazili, Oktoba 16, 2022. © Marcelo Chello/AP
Matangazo ya kibiashara

Haijulikani iwapo mdahalo wa kitamaduni wa televisheni ya Globo utakuwa wa maamuzi, lakini pengo likiwa dogo sana kati ya wagombea hao wawili, hakika litakuwa na ushawishi kwenye matokeo. Hii ndiyo sababu Lula na Jair Bolsonaro watapitia faili zao siku nzima. Watazungukwa na washauri, ambao watawaeleza kwa kifupi, kuwaambia wakati wa kuwa mkali zaidi, au wakati, kinyume chake, kubaki mtulivu.

Inafahamika kwamba Jair Bolsonaro ni gwiji katika sanaa ya uchochezi - anapenda sana kumwita Lula "fisadi", au "mfungwa wa zamani". Kuhusu Lula, hivi majuzi alimwita rais "mnyanyasaji". Inabakia kuonekana atafikia wapi wakati wa mjadala huu, au ikiwa atatumia tu mada ya uhaba wa chakula nchini. Na kisha, katika mkesha wa mjadala huu, Lula alichapisha programu ndogo yenye pointi 13, ambayo inaanzia kwa uchumi hadi sera ya kigeni - kwa niaba ya wale ambao, hasa, walimkosoa kwa kutokuwa wazi katika mapendekezo yake.

Kura zinazokaribiana

Katika uchaguzi huo, Lula atakuwa karibu pointi 6 mbele ya mpinzani wake, kulingana na Taasisi ya Datafolha, ambayo ilichapisha kura siku ya Alhamisi jioni. Mwenendo huo ni mzuri kwa Lula, kwani wiki moja iliyopita pengo lilikuwa la alama 4 tu. Takwimu hizi, kwa kweli, zinafanana sana na matokeo ya duru ya kwanza ambapo Lula alikuwa mbele ya mpinzani wake kwa pointi 5. Hii itamaanisha kwamba baada ya wiki nne za kampeni zisizo na huruma, mara nyingi za uchokozi, mwelekeo wa duru ya kwanza unaendelea: Lula hakujazia pengo lake na Bolsonaro alishindwa kukamilisha muda aliyopoteza.

Wananchi wa Brezil wanasubiri kuona nani atachukuwa nafasi nzuri ya kuliongoza taifa lao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.