Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais Brazil: Lula na Bolsonaro kumenyana katika duru ya pili

Rais wa zamani wa mrengo wa kushoto Lula aliibuka kidedea katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Brazil Jumapili, dhidi ya rais anayemaliza muda wake, wa mrengo wa kulia Jair Bolsonaro, lakini ushindi wake ni mdogo ikilinganishwa na jinsi ilivyotabiriwa. Duru ya pili itafanyika Oktoba 30.

Luiz Inacio Lula da Silva na Jair Bolsonaro watamenyana duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Brazil Oktoba 30.
Luiz Inacio Lula da Silva na Jair Bolsonaro watamenyana duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Brazil Oktoba 30. AFP - EVARISTO SA
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa tume ya uchaguzi nchini Brazil wamesema kuwa duru ya pili ya uchaguzi itafanyika Oktoba 30, baada ya wagombea wawili wakuu kushindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zinazohitajika.

Luiz Inacio Lula da Silva, mwanasiasa kongwe wa mrengo wa kushoto nchini Brazil, alishinda 48.43% ya kura, dhidi ya rais anayemaliza muda wake, aliyepata 43.20%, Mahakama ya Juu ya Uchaguzi (TSE) ilitangaza jana jioni, kulingana na kura zilizohesabiwa kutoka 99.99% ya vituo vya kupigia kura.

Ushindi huu mwembamba unamkatisha tamaa Lula, ambaye utabiri wake ulibaini ushindi mkubwa, tena katika duru ya kwanza. Atalazimika kukabiliana na mshindani wake katika duru ya pili mnamo Oktoba 30, kama ilivyoainishwa na sheria ya uchaguzi.

"Pambano linaendelea hadi ushindi wa mwisho", amesema rais wa zamani wa mrengo wa kushoto. "Tutashinda uchaguzi huu," amesema Lula, akiahidi "safari zaidi, mikutano mingine" kukutana na Wabrazili kushinda muhula wa tatu kwa sababu, amesema, "tunahitaji nchi hii kuinuka katika nyanja zote".

"Nitapata fursa ya kujadili kwa mara ya kwanza na rais, kujua kama ataendelea kueneza uongo au kama - kwa mara ya kwanza - atakuwa mwaminifu kwa watu wa Brazil," ameongeza Lula. Ni nafasi ambayo raia wa Brazil wananipa. Na ninataka kuwambia kuwa ninaanza kampeni yangu ya duru ya pili kesho. "

Utawala wa Bolsonaro umegubikwa na hotuba zenye utata au uchochezi, hujuma dhidi ya taasisi za kidemokrasia, ukosoaji mkubwa dhidi yake kwa namna alivyoshughulikia janga la COVID na uharibifu mkubwa wa msitu wa mvua wa Amazon katika miaka 15 iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.