Pata taarifa kuu
MAREKANI

Angela Merkel akutana na Joe Biden kwa mazunumzo Washington

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Marekani Joe Biden wamekutana kwa mazungumzo, hasa Angela Merkela akija kumuaga kuwa hivi karibuni ataachia ngazi na kumpisha mrithi wake.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel almepokelewa na mwenyeji wake Joe Biden katika Ikulu ya White House Alhamisi Julai 15, 2021.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel almepokelewa na mwenyeji wake Joe Biden katika Ikulu ya White House Alhamisi Julai 15, 2021. REUTERS - TOM BRENNER
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili wamesisitiza juu ya hitaji la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao mbili kwa miezi na miaka ijayo. Wametia saini tamko la pamoja ambalo linakumbusha maadili yanayowakutanisha, na wakakukabiliana nchi zao kuendelea kuwa kitu kimoja dhidi ya changamoto kubwa zinazoikabili dunia, lakini wameonyesha pia kutokubaliana kwao, hasa kuhusu bomba la gesi la Nord Stream ambalo litaiwezesha Ujerumani kupata nishati kutoka Urusi.

Mataifa mengine pia wanachama wa Jumuiya ya Kujihami NATO wanaupinga mradi huo wa bomba la gesi.

"Kansela anaifahamu ofisi hii kama mimi," Joe Biden ametania kabla ya kusifu kazi ya kipekee ya Angela Merkel, ambaye amehudumu kwa miaka mingi sawa na mihula ya marais wanne wa Marekani. Ataondoka madarakani mwishoni mwa mwaka huu. Ni kiongozi wa kwanza wa Ulaya kukaribishwa katika Ikulu ya White House tangu uchaguzi wa Joe Biden.

Ujerumani na Marekani kuimarisha zaidi mahusiano yao

Kansela Merkel amefanya ziara 20 nchini Marekani katika muhula wake wa miaka 16 na amekutana na marais wanne wa taifa hilo tangu alipoingia madarakani mnamo 2005.

Angel Merkel amenuwia kuimarisha tena mahusiano kati ya Berlin na Washington yaliyopwaya enzi ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump.

Biden amemshukuru Kansela Merkel kwa uongozi wake na kusema wakati anajitayarisha kuwachia wadhifa huo baada ya  miaka 16 ya kuiongoza Ujerumani, mahusiano kati ya nchi hizo mbili yataendelea kuwa imara chini ya misingi aliyoijenga.

Viongozi hao wawili kwa pamoja wameahidi nia yao ya kushirikiana kwa karibu kuhimiza amani, usalama na ustawi kote duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.