Pata taarifa kuu
G 7-UINGEREZA

Viongozi kutoka mataifa tajiri ya G7 waja na mpango wa kufadhili miundombinu

Viongozi wa mataifa tajiri duniani ya G7, wamekuja na mpango wa kusaidia mataifa yenye kipato cha chini na kati, kujenga miundo mbinu mizuri na imara.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron  akikutana na rais wa Marekani Joe Biden Juni 12 2021 pembezoni mwa kikao cha G 7 nchini Uingereza
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana na rais wa Marekani Joe Biden Juni 12 2021 pembezoni mwa kikao cha G 7 nchini Uingereza REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Joe Biden amesema anataka mpango wa Marekani wa Build Back Better World (B3W) kujenga miundo mbinu bora ili kuyavutia mataifa hayo ambayo yameonekana kuegemea upande wa China ambao umekuwa ukifadhili ujenzi wa barabara reli, reli na bandari katika mataifa mengi.

Hata hivyo, haijafahamika ni namna gani mpango huo utafadhiliwa wakati huu viongozi hao wakikutana kwa siku ya pili leo katika eneo la Carbis Bay mjini Cornwall.

Aidha, katika siku ya pili ya kikao hicho, mwenyeji wa kikao hiki, Waziri Mkuu Boris Johnson alikutana na kufanya mazungumzo na rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Angela Markel na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya.

Rais Macron amemwabia Johnson kuwa, nchi yake iko tayari kuimarisha tena mahusiano kati ya nchi hizo mbili, iwapo Uingereza itaheshimu mkataba wa Brexit, ambao nchi hiyo ilijiondoa kwenye umoja wa Ulaya.

 

Rais  Emmanuel Macron akiwa na Waziri Mkuu  Boris Johnson, pembezoni mwa kikao cha  G7.
Rais Emmanuel Macron akiwa na Waziri Mkuu Boris Johnson, pembezoni mwa kikao cha G7. © AFP - LUDOVIC MARIN

Tangu Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya mwaka uliopita, mahusiano kati yake na mataufa ya Ulaya hasa Ufaransa, yamekuwa mabaya.

Rais Macron amekuwa akiishtumu Uingereza kwa kwa kukataa kuheshimu mkataba huo wa Brexit wakati hu Macron akimsisitizia Johnson kuwa nchi hizo mbili zina maslahi sawa, lakini mahusiano yataimarishwa tu kwa Uingereza kuheshimu mkataba huo.

Katika hatua nyingine, Johnson ambaye amekuwa akikutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya, ametishia kufuta makubaliano ya baada ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, kuhusu ufanyaji biashara kati ya Ireland Kaskazini na EU iwapo viongozi hao wa Ulaya wataendelea kumshinikiza kuhusu mkataba huo.

Viongozi wa mataifa hayo tajiri duniani, baadaye wanatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja kuhusu masuala waliyojadiliana ikiwa ni pamoja na namna ya kuisadia dunia kupata chanjo za kuzuia maambukizi ya Covid 19, suala la mabadiliko ya tabia nchi, miongoni mwa mambo mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.