Pata taarifa kuu
MAREKANI

Marekani kupeleka wanajeshi 500 zaidi nchini Ujerumani

Marekani itaongeza askari 500 kwa kikosi chake kilichoko Ujerumani , Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema Jumanne wakati wa ziara yake mjini Berlin.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na mwenzake wa Ujerumani Annegret Kramp-Karrenbauer wakihutubia mkutano na waandishi wa habari huko, Bendlerblock makao makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani huko Berlin, Ujerumani, Aprili 13, 2021.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na mwenzake wa Ujerumani Annegret Kramp-Karrenbauer wakihutubia mkutano na waandishi wa habari huko, Bendlerblock makao makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani huko Berlin, Ujerumani, Aprili 13, 2021. REUTERS - KAY NIETFELD
Matangazo ya kibiashara

Ahadi hii ni mabadiliko kamili na mpango wa Donald Trump wa kuwatoa karibu askari 12,000 wa Marekani kutoka Ujerumani, ambapo rais wa zamani wa Marekani aliituhumu Ujerumani kutokuheshimu ahadi zake za bajeti ya ulinzi katika Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO.

"Tumemaliza mpango (wa kuondoa askari)," Lloyd Austin amesema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Ujerumani Annegret Kramp-Karrenbauer.

"Nadhani jukumu la askari 500 wa ziada linashuhudia kiwango cha ushirikiano wetu na kujitolea kwetu kwa NATO," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.